bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Timothy 2
1 Timothy 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 3 →
1
*Neno, ninalokuhimiza kupita yote, ni hili: Mwombe na kumwangukia Mungu na kumbembeleza na kumshukuru mkiwaombea watu wote,
2
nao wafalme nao wote walio wakuu, tupate kukaa tukitulia na kutengemana vema, tumche Mungu na kuendelea vema katika mambo yote.
3
Kwani hivi ni vizuri vya kumpendeza Mungu, mwokozi wetu.
4
Huyu anataka, watu wote waokolewe, wapate kutambua yaliyo ya kweli.
5
Kwani Mungu ni mmoja, naye mpatanishaji wa Mungu na watu ni mmoja, ni yule mtu Kristo Yesu
6
aliyejitoa mwenyewe kuwa kole ya kuwakomboa wote; huu ndio ushuhuda utakaotangazwa po pote, siku zake zitakapotimia.*
7
Nami nimewekewa kuwa mtangazaji na mtume wake, nasema kweli, sisemi uwongo, niwe mfunzi wa wamizimu, niwafundishe kumtegemea Mungu na kuyashika yaliyo ya kweli.
8
Nataka, waume wamwombe Mungu mahali pote wakiinua mikono itakatayo, pasipo kukasirika na kuchokoza.
9
Vivyo hivyo nataka, penye kuomba wanawake wavae mavazi yafaayo wakijipamba, kama iwapasavyo wenye soni waonyekao; mapambo yao yasiwe misuko ya nywele wala dhahabu wala ushanga wala nguo zilizo za mali nyingi.
10
Ila mapambo yao yawe matendo mema yawapasayo wanawake wanaoungama kuwa wake Mungu!
11
Mwanamke sharti ajifunze kutulia na kutii sana!
12
Lakini simpi mwanamke ruhusa kufundisha, wala kumtawala mumewe, ila akae na kutulia.
13
Kwani Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, halafu Ewa.
14
Naye Adamu siye aliyedanganyika, ila mwanamke ndiye aliyedanganyika, akatangulia kukosa.
15
Lakini ataokoka kwa kuzaa watoto, hao wakiwa wenye kumtegemea Mungu na wenye kupendana na wenye kutakaswa mioyo na wenye kuonyeka.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6