bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Timothy 5
1 Timothy 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 6 →
1
Aliye mzee usimkaripie, ila umbembeleze, kama ni baba yako! Walio waume wazima useme nao, kama ni ndugu zako!
2
Wanawake wazee nao uwabembeleze, kama ni mama zako! Walio wake wazima useme nao na kuyaangalia yote yenye soni, kama ni dada zako!
3
Wanawake wajane walio wajane kweli uwaheshimu!
4
Lakini mwanamke mjane akiwa na watoto au wajukuu, basi, hao wajifunze kwanza kuwaheshimu walio nao nyumbani mwao wenyewe, wakiwalipa wamama na wabibi mema, walioyapata kwao! Kwani hivi vinapendezeka mbele ya Mungu.
5
Lakini aliye mjane wa kweli ni yule aliyeachwa peke yake tu; yeye humngojea Mungu akifuliza kumwomba Mungu na kuwaombea wengine usiku na mchana.
6
Lakini anayezifuata tamaa zake huyo amekwisha kufa akingali yupo bado.
7
Mambo haya uyaagize, watu wasione neno la kuwaonya!
8
Lakini mtu asipowatunza walio ndugu zake, kupita wengine wale waliomo nyumbani mwake, basi, huyo amekwisha kumkana, aliyemtegemea, naye ni mwovu kuliko wale wasiomtegemea Mungu.
9
Mwanamke mjane apaswaye na kuandikiwa ujane ni yule aliyemaliza miaka 60, aliyekuwa mke wa mume mmoja;
10
nayo matendo yake sharti yajulikane kuwa mazuri, kama kukuza watoto au kupenda wageni au kuosha watakatifu miguu au kusaidia wenye maumivu au kufuata matendo mema yawayo yote.
11
Lakini wajane, wasiomaliza bado ile miaka, uwakatae! Kwani hao wangawa wamtumikia Kristo, watakapoingiwa na tamaa ya mume, wanataka kuolewa,
12
ijapo wajiumbue kwamba: Hivyo, walivyomtegemea Mungu kwanza, wamevitangua.
13
Vilevile hujizoeza kuwa wavivu na kutangatanga nyumba kwa nyumba. Nao si wavivu tu, ila wanao upuzi mwingi, hunyatia wengine, husema yasiyopasa.
14
Kwa hiyo nataka, wasio wazee waolewe, wazae watoto, wayaangalie mambo ya nyumbani mwao, mpingani wasimsengenyeshe,
15
kwani hivyo wako waliogeuka wakimfuata Satani.
16
Lakini mwanamke mwenye kumtegemea Mungu akiwa na wajane mwake, na awatunze, wateule wasilemewe, wapate kuwatunza walio wajane kweli.
17
Wazee wanaosimamia vizuri sharti wapewe heshima mara mbili, kupita wengine ni wale wanaojisumbua kulitumikia lile Neno kwa kulifundisha.
18
Kwani Maandiko yasema: Ng'ombe mwenye kupura ngano usimfunge kinywa! Na tena: Mtenda kazi hupaswa na kupewa mshahara wake.
19
Mzee akisutwa, ukatae, wasipokuwapo mashahidi wawili au watatu!
20
Wakosao uwaonye mbele yao wote, wale wengine nao wapate kuogopa!
21
Namtaja Mungu na Kristo Yesu nao malaika waliochaguliwa kuwa mashahidi nikikuagiza sasa, uyashike maneno haya, nalo utakalolifanya lo lote, ulifanye pasipo kuchukizwa wala pasipo kupendezwa na mtu!
22
Usimbandikie mtu mikono upesi! Wala usijitie katika makosa ya wengine! Jiangalie, uwe mng'avu!
23
Usifulize kunywa maji tu, ila utumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako, likipatwa na manyonge mara kwa mara!
24
Watu wengine makosa yao yako waziwazi, huwaongoza na kuwapeleka penye hukumu; lakini wengine makosa yao hutokea nyuma yao.
25
Vivyo hivyo nayo matendo mazuri mengine yako waziwazi; nayo yasiyo waziwazi hayafichiki.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6