bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Timothy 3
1 Timothy 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 4 →
1
Neno hili ni la kweli: Mtu akitaka kazi ya ukaguzi anataka kazi nzuri.
2
Mkaguzi sharti awe mtu asiye na neno la kimkanya, mwenye mke mmoja, asiyekunywa kileo, mwerevu wa kweli, mwema, mpenda wageni, ajuaye kufundisha.
3
Asikae na wanywaji, asiwe mgomvi, ila awe mpole, pasipo matata na pasipo choyo;
4
ajue kuiangalia vizuri nyumba yake mwenyewe, hata watoto wake wawe wenye kutii na kuwapa watu wote macheo.
5
Maana mtu asiyeweza kuiangalia nyumba yake mwenyewe atawezaje kuwatunza wateule wa Mungu?
6
Mtu aliye Mkristo mpya asiwe mkaguzi, asijitutume, akaja kuanguka katika hukumu ya Msengenyaji.
7
Nao walioko nje sharti wamshuhudie kuwa mwema, asije kusingiziwa mabaya, akanaswa na tanzi la Msengenyaji.
8
Vivyo hivyo nao watumikiaji wa wateule wawe wenye macheo, wasiosema kuwili, wasio walewi, wasiofuata machumo mabaya,
9
ila waliangalie lile fumbo walitegemealo katika mioyo itakatayo kwa kujua tu yaliyo mema.
10
Hao kwanza wajaribiwe! Ikijulikana, ya kuwa haliko neno la kuwakamia, basi, wawekwe kuwa watumikiaji.
11
Vivyo hivyo nao wake zao wawe wenye macheo wasiosengenya, wasiokunywa kileo, walio waelekevu katika mambo yote!
12
Watumikiaji sharti wawe kila mtu mume wa mke mmoja, wenye kuwaangalia vizuri watoto wao na nyumba zao wenyewe.
13
Kwani waliotumika vizuri hujipatia fungu zuri, tena kwa hivyo, wanavyomtegemea Kristo Yesu, huona furaha nyingi kwa kumtangaza.
14
Nakuandikia haya, ijapo nangojea, bado kidogo nifike kwako.
15
Lakini kama nakawia, ujue mwenendo unaopasa katika nyumba ya Mungu! Hiyo nyumba ndio wateule wake Mungu aliye Mwenye uzima; nao ndio nguzo na msingi wa kuyashikiza yaliyo ya kweli.
16
Kweli fumbo lililo kuu ni lile la kumcha Mungu: Mungu alitokea waziwazi mwilini, akapata wongofu kwa kuwa mwenye Roho, akaonekana penye malaika, akatangazwa kwa wamizimu, akategemewa ulimwenguni, akapazwa mbinguni kwenye utukufu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6