bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Timothy 4
1 Timothy 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 5 →
1
Lakini Roho anasema waziwazi: Siku za mwisho watakuwako watakaoacha kumtegemea Mungu, wakifuata rohoroho za upotevu na mafundisho ya mapepo:
2
ndio watu waliodanganywa nao wanaojitendekeza kwa kusema uwongo na kwa kuficha, ya kuwa wenyewe wamechomwa moto mioyoni kwa kufanya hivyo.
3
Ndio wanaokataza watu kuoa, tena hutangaza miiko ya vyakula, Mungu alivyoviumba, wavile na kushukuru, wakiwa wenye kumtegemea na kuyatambua yaliyo ya kweli.
4
*Kwani kila kilichoumbwa na Mungu ni kizuri, wala hakuna chenye mwiko kinacholiwa, watu wakimshukuru.
5
Kwani kinatakaswa kwa neno lake Mungu, watu wanapokiombea.
6
Ukiwafundisha ndugu mambo hayo utakuwa mtumishi mzuri wa Kristo Yesu, nawe utajilisha maneno, tuyategemeayo, tunayoyafundisha kwamba: Ni mazuri; ni hayo, uliyoyafuata nawe.
7
Lakini yale masimulio yasiyo na maana, yapendezayo wazee wa kike tu, yakatae! Jizoeze kumcha Mungu!
8
Kwani mazoezo ya mwili hufalia mambo machache tu; lakini kumcha Mungu hufalia mambo yote, tena kunacho kiago cha uzima wa sasa na cha ule utakaokuwapo.
9
Neno hili ni la kweli, nalo linapasa kushikwa na watu wote.
10
Kwani kwa sababu hii twasumbuka tukigombezwa, ya kuwa tumemngojea Mungu Mwenye uzima aliye mwokozi wa watu wote, kwanza wao wamtegemeao.
11
Mambo haya uyaagize na kuyafundisha!*
12
Mtu asikubeze kwamba: U kijana bado! Ila wenye kumtegemea Mungu uwe kielezo chao cha kujifundishia kusema na kuendelea na kupendana na kumtegemea Mungu na kujitakasa.
13
Mpaka nitakapofika, ufulize kuwasomea na kuwaonya na kuwafundisha!
14
Usiache kuyatunza yale mema, uliyogawiwa kwa kufumbuliwa kwanza, kisha ukayapata kwa kubandikiwa mikono ya wazee.
15
Mambo hayo uyatunze, ushikamane nayo, wote wapate kuona, unavyoendelea!
16
Jiangalie mwenyewe, uyaangalie nayo, unayoyafundisha, ujikaze yayo hayo! Kwani ukiyafanya hayo utajiokoa mwenyewe, hata wanaokusikia.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6