bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Timothy 6
1 Timothy 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
1
Wote walio katika mafungo ya utumwa sharti wawape mabwana zao heshima zote, Jina la Mungu nao ufundisho wetu usifyozwe!
2
Lakini walio wa mabwana wenye kumtegemea Mungu wasiwabeze, kwa kwamba ni ndugu, ila wawatumikie kupita wengine, kwa sababu nao wamemtegemea Mungu! Inafaa, wapendwe, maana nao hutaka kuwafanyizia kazi njema.
3
Mtu akifundisha mengine, asiposhikamana na maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo yatupayo uzima wala na ufundisho upasao wenye kumcha Mungu,
4
basi, mtu huyo ametutumka, hana, akijuacho, kilema chake ni mashindano na mabishano ya kujisemea tu. Hayo ndiyo yanayoleta wivu na ugomvi na matusi na masingizio mabaya
5
na machukivu yasiyokoma. Hao huwa kama wenye wazimu waepukao kabisa kwenye kweli, ndio wanaodhani kwamba: Kumcha Mungu ni chumo. Walio hivyo jitenge nao!
6
*Kweli kumcha Mungu ni chumo kubwa, kukiwa pamoja na kutoshewa nayo, tuliyo nayo.
7
Kwani hakuna, tulichokileta humu ulimwenguni, wala hakuna, tuwezacho kutoka nacho tena.
8
Lakini tukiwa na vyakula na vya kuvaa tuseme: Vinatutoshea!
9
Lakini wanaotaka kupata mali nyingi huanguka penye majaribu na matanzi na tamaa nyingi zisizo na maana, ziponzazo watu na kuwatumbukiza maangamizoni, wanapopata kuoza tu.
10
Kwani choyo ni shina la maovu yote. Wengine walikifuata, wakapotelewa, wasiweze kumtegemea Mungu tena, wakajipatia maumivu mengi.
11
Lakini wewe uliye mtu wa Mungu hayo yakimbie! Ukimbilie wongofu na kumcha Mungu na kumtegemea na kupendana na kuvumilia na kujinyenyekeza!
12
Vipige vile vita vizuri vya kumtegemea Mungu! Ishike njia ya uzima wa kale na kale, ulioitiwa, ukaungama ungamo zuri mbele ya mashahidi wengi.*
13
Nakuagiza mbele yake Mungu anayevipa vyote uzima na mbele ya Kristo Yesu aliyelishuhudia ungamo lake zuri mbele ya Pontio Pilato,
14
uyalinde uliyoagizwa, yasiwe na doadoa wala kilema, mpaka bwana wetu Yesu Kristo atakapotokea;
15
naye atakayemtokeza kwetu, siku zake zitakapotimia, ni yule anayeshangiliwa kuwa Mwenyezi peke yake, yule mwenye kutawala wafalme na mabwana.
16
Ni yeye peke yake asiyekufa, hukaa mwangani, msimofikiwa na mtu; hakuna mtu aliyemwona, wala hakuna awezaye kumtazama. Yeye aheshimiwe, kwa sababu nguvu ni zake kale na kale! Amin.
17
Walio wenye mali nyingi humu ulimwenguni waagize, wasijikweze, wala wasizitumainie mali, maana hutoweka upesi; ila sharti wamtumainie Mungu anayetupatia yote na kuyafurikisha, tushibe vema.
18
Waagize, wafanye mwenendo mwema wakifuliza kufanya kazi nzuri, wakigawia wengine mema yao kwa kuwa bia moja nao.
19
Hivyo ndivyo, watakavyojiwekea malimbiko yatakayokuwa msingi mzuri, siku zitakapotimia za kuupata uzima ulio wa kweli.
20
Timoteo, yalinde, uliyopewa ya kuyaweka! Yakatae yale mapuzi yaliyo ya bure tu nayo yale mabishano ya utambuzi ulio wa uwongo tu!
21
Maana wengine walioufuata wamepotelewa na njia ya kumtegemea Mungu. Upole uwakalie ninyi! Amin.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
All chapters:
1
2
3
4
5
6