bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
James 1
James 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
1
Mimi Yakobo niliye mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo nawasalimu ninyi mlio mashina kumi na mawili yaliyotawanyika.
2
Ndugu zangu, mnapotumbukia katika majaribu yaliyo mengi na mengi yawazieni kuwa machangamko tu!
3
Yatambueni: Kumtegemea Mungu kukijulishwa hivyo kuwa kwa kweli huwaletea uvumilivu.
4
Nao uvumilivu sharti uitimize kazi yake, ninyi mpate kutimilika, mwe Wakristo wazima wasioachwa nyuma katika jambo lo lote.
5
Lakini kama kwenu yuko akosaye werevu wa kweli, na amwombe Mungu anayependezwa kuwapa watu wote pasipo mawazo ya kinyuma; ndipo, atakapopewa.
6
Lakini sharti aombe kwa kumtegemea, asiwe na mambo mawili moyoni! Kwani mwenye mambo mawili hufanana na wimbi la bahari linalorushwarushwa na upepo na kutupwatupwa.
7
Mtu aliye hivyo asidhani, ya kuwa kiko, atakachokipata kwake Bwana!
8
Mtu mwenye mioyo miwili hugeukageuka katika njia zake zote.
9
Lakini ndugu mnyenyekevu na ajivunie ukuu wake,
10
naye mwenye mali na ajivunie unyenyekevu wake, kwani atanyauka kama maua ya majani.
11
Kwani jua likicha na kuwaka kwa ukali huyakausha majani, maua yaanguke, uzuri wao uliofurahisha macho uangamie. Vivyo hivyo naye mwenye mali hunyauka katika mienendo yake.
12
Mwenye shangwe ni mtu anayevumilia akijaribiwa. Kwani akiisha kushinda atapewa kilemba chenye uzima, Mungu alichowaagia wale wampendao.
13
Mtu akijaribiwa asiseme: Najaribiwa na Mungu! Kwani Mungu hajaribiki nayo maovu, naye mwenyewe hajaribu mtu.
14
Ila kila mtu hujaribiwa akivutwa na kuhimizwa na tamaa yake mwenyewe.
15
Kisha tamaa ikijitunisha huzaa makosa, nayo makosa yakikomaa huzaa kufa.
16
*Msidanganyike, ndugu zangu wapendwa!
17
Kila kipaji kizuri na kila gawio timilifu hutoka juu kwa Baba alie mwenye mianga. Yeye hageuki, wala kwake hakupokeani mwanga na giza.
18
Kwa hayo, ayatakayo, alituzaa sisi kwa nguvu ya Neno lililo kweli, tupate kuwa kama malimbuko ya viumbe vyake.
19
Mwajua, ndugu zangu wapendwa: kila mtu awe mwepesi, apate kusikia, lakini awe mpole, asiseme upesi, tena mpole, asipatwe na makali upesi!
20
Kwani makali ya mtu hayafanyi yaongokayo mbele ya Mungu.
21
Kwa hiyo uvueni uchafu wote na ule uovu mwingi uliowashika! Lipokeeni kwa upole Neno lililopandwa mwenu, liwezalo kuziokoa roho zenu!*
22
*Mwe wafanyaji wa Neno, msiwe wasikiaji tu! Kwani hivyo mwajidanganya wenyewe.
23
Kwani mtu akiwa msikiaji wa Neno, asiwe hata mfanyaji, huyo amefanana na mtu aliyetazama katika kioo, uso wake ulivyo;
24
akiisha kujitazama huenda zake, akasahau upesi, alivyokuwa.
25
Lakini achunguliaye, aone, Maonyo yalivyotimilika hapo, tulipokombolewa, akishikamana navyo, hawezi kuwa msikiaji asahauye upesi, aliyoyasikia, ila huwa mfanyaji wa kazi yake, naye atakuwa mwenye shangwe kwa kule kufanya kwake.
26
Mtu akijiwazia kuwa mwenye kumtumikia Mungu, lakini haushindi ulimi wake, anaudanganya moyo wake mwenyewe, kwa hiyo matumikio yake ni ya bure.
27
Matumikio yatakatayo yasiyo yenye doa hata machoni pa Mungu Baba ndiyo haya: kukagua watoto waliofiwa na wazazi na kukagua nao wanawake wajane katika maumivu yao na kujilinda wenyewe, tusijitie katika machafu ya ulimwwengu huu.*
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5