bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
James 4
James 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
1
Magomvi yenu ya kupigana ninyi kwa ninyi yanatoka wapi? Sipo hapo, mzichezeapo tamaa zenu zinazoshindana katika viungo vyenu?
2
Mwakifuata kijicho, lakini hampati; mwauana kwa wivu, lakini hamwezi kuyafikia, myatakayo; mwapigana na kugombana, lakini hamna kitu, kwa sababu hamwombi.
3
Mngawa mwaomba, lakini hampewi, kwa sababu mwaomba vibaya, maana mwataka tu ya kutumia katika machezo yenu.
4
Enyi wazinzi waume na wanawake, hamjui: kuupenda ulimwengu huu ni kuchukiwa naye Mungu? Anayetaka kuwa mpenzi wa ulimwengu huu, hugeuka kuwa mchukivu wa Mungu.
5
Au mwawaza, ya kuwa Maandiko yanasema bure: Roho aliyekaa ndani yetu anataka sana kushindana na wivu?
6
Nayo mema, atugawiayo, ni makubwa kuushinda. Kwa hiyo maandiko yasema: Wenye kujikweza Mungu huwapingia, lakini wanyenyekevu huwapatia huruma.
7
Kwa hiyo mtiini Mungu! Satani mbisheni! Ndivyo, atakavyowakimbia.
8
Mkaribieni Mungu! Ndivyo, atakavyowakaribia nanyi. Enyi wakosaji, ing'azeni mikono! Enyi wenye mioyo miwili, itakaseni mioyo!
9
Jisumbueni na kusikitika na kuomboleza! Macheko yenu yageuke kuwa vilio, nazo furaha zenu zigeuke kuwa masikitiko!
10
Mjinyenyekeze mbele ya Bwana! Ndivyo, atakavyowakuza ninyi.
11
Msitetane, ndugu! Anayemteta ndugu au anayemwumbua ndugu yake huyateta Maonyo na kuyaumbua Maonyo. Lakini ukiyaumbua hu mfanyaji wa Maonyo, ila muumbuzi.
12
Mwenye kuyatoa Maonyo na mwenye kuhukumu ni mmoja, maana ni yeye anayeweza kuokoa na kuangamiza. Lakini wewe u nani ukimwumbua mwenzio?
13
*Sasa tusemeane nanyi mnaosema: Leo au kesho tutakwenda mjini fulani, tukae huko mwaka mzima, tuchuuze na kuchuma!
14
Nanyi hamjui, itakayokuwa kesho. Kuishi kwenu ni kwa namna gani? Maana ninyi m kama mvuke unaoonekana kitambo kidogo, kisha hutoweka.
15
Mngesema: Bwana akitaka, tutaishi, tufanye hivi na hivi.
16
Lakini sasa mwajivunia kwa kujitutumua; majivuno yote yaliyo hivyo ni mabaya.
17
Ajuaye kufanya mazuri, asiyafanye, amekwisha kukosa.*
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5