bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
James 5
James 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
1
Sasa tusemeane nanyi wenye mali: Lieni na kuyaombolezea mahangaiko yenu yatakayowapata!
2
Mali zenu zimeoza, nguo zenu zimeliwa na mende.
3
Dhahabu zenu na fedha zenu zimeingiwa na kutu, nazo kutu zao zitawasuta, zitawala nyama za miili yenu kama moto. Mmelimbika mali nyingi siku hizi za mwisho.
4
Angalieni, malipo, mliyowanyima wakulima wa mashambani kwenu, yanalia, nayo malalamiko ya wavunaji yamefika masikioni mwa Bwana Mwenye vikosi.
5
Mmeyala mazuri yaliyoko nchini na kutapanya mali. Mioyo yenu mmeinonesha siku za kuchinja nyama.
6
Mwongofu mmemhukumu, mkamwua; naye hakuwabishia.
7
Ndugu, vumilieni, mpaka Bwana atakaporudi! Tazameni, mkulima anavyoyangoja mazao ya nchi, maana ni yenye kima! Huvumilia mpaka apate mvua ya vuli nayo ya masika.
8
Vumilieni nanyi, mwitie mioyo yenu nguvu! Kwani kurudi kwake Bwana kumekaribia.
9
Ndugu, msinung'unikiane ninyi kwa ninyi, msipate kuhukumiwa! Tazameni, mhukumu amesimama milangoni mwenu!
10
Ndugu, wafumbuaji waliosema kwa nguvu ya Jina la Bwana washikeni kuwa vielezo vya kujifunzia kuteseka vibaya na kuvumilia!
11
Tazameni, twawatazamia wavumiliao kuwa wenye shangwe! Mmesikia, Iyobu alivyovumilia, nao mwisho wa Bwana mmeuona, kwani Bwana huonea wengi uchungu na upole.
12
Ndugu zangu, nilitakalo sana, ni hili la kwamba: Msiape! Msiape na kutaja wala mbingu wala nchi wala kiapo kingine cho chote! Mkisema: Ndio, iwe ndio kweli. Tena mkisema: Sio, iwe sio kweli, kwamba msitumbukie hukumuni!
13
*Kwenu kama yuko mwenye kuteseka, na amwombe Mungu! Kama yuko mwenye kutulia, na aimbe nyimbo!
14
Kama yuko mwenye kuugua, na awaite wazee wa wateule, wamwombee, tena wampake mafuta katika Jina la Bwana!
15
Wakimwombea kwa kumtegemea Mungu, vitamwokoa yule mgonjwa, naye Bwana atamwinua tena; kama yuko na makosa, aliyoyafanya, ataondolewa.
16
Jiungamianeni makosa ninyi kwa ninyi na kuombeana, mpate kupona! Kuomba kwake mwongofu kuko na nguvu nyingi kukiwa kwa kweli.
17
Elia alikuwa mtu aliyeteseka kama sisi; naye alipomwomba Mungu, mvua isinye, ndipo, mvua ilipoacha kunya nchini miaka mitatu na miezi sita.
18
Alipoomba tena, ndipo, mbingu ziliponyesha mvua, nayo nchi ikayachipuza mazao yake.
19
Ndugu zangu, kama kwenu yuko aliyepotea na kuyaacha yaliyo ya kweli, tena mwingine akimrudisha,
20
tambueni: mwenye kurudisha mkosaji, aiache ilenjia yake ya upotevu, huiokoa roho yake kufani na kufunika makosa mengi!*
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
All chapters:
1
2
3
4
5