bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
James 2
James 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 3 →
1
Ndugu zangu, msiwaze kwamba: Kumtegemea Bwana wetu mtukufu Yesu Kristo hupatana na kupendelea watu!
2
Ni hivyo: mle mkutaniamo mkiingia mtu mwenye pete za dhahabu vidoleni, aliyevaa mavazi mazuri, tena mkiingia hata maskini mwenye mavazi machakavu,
3
nanyi mkamtazama yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia: Wewe kaa hapa pazuri! kisha mkamwambia yule maskini: Wewe simama huko au kaa hapa chini miguuni pangu!
4
je? Hivyo mioyo yenu haikujiumbua kwamba: Mkiwagawanya hivyo mmefuata mawazo mabaya?
5
Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa! Mungu hakuwachagua walio maskini ulimwenguni, wawe wenye mali kwa kumtegemea, tena wautwae ufalme, aliowaagia wampendao, uwe urithi wao?
6
Lakini ninyi mmemnyima maskini heshima. Wenye mali sio wanaowaendea ninyi kwa nguvu? Sio wanaowaburura bomani?
7
Nao sio wanaolitukana lile Jina zuri, mwitwalo nalo?
8
Kweli, mkilitimiza Agano la kifalme, kama lilivyoandikwa kwamba: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe! mnafanya vizuri.
9
Lakini mkiwapendelea watu mnakosa, mkajulishwa na hilo agizo waziwazi kuwa wenye kulipita.
10
*Kwani mtu akiyashika Maonyo yote akalikosea moja tu, amekwisha kuyakosea yote.
11
Kwani yeye aliyesema: Usizini! ndiye aliyesema: Usiue! Nawe usipozini, lakini unaua, basi, umekwisha kuwa mwenye kuyapita Maonyo.
12
Semeni, tena fanyeni hivyo, kama watu wafanyavyo watakaohukumiwa kwa Maonyo yanayotupatia kukombolewa!
13
Kwani mtu akosaye huruma atapata naye hukumu ikosayo huruma; lakini huruma hushangilia nako kwenye hukumu.
14
Ndugu zangu, mtu akisema: Niko na kumtegemea Mungu, lakini matendo hanayo, inamfaliaje? Kumtegemea Mungu kunaweza kumwokoa?
15
Kwetu kukipatikana ndugu mume au mke walio wenye uchi na wenye kukosa chakula cha siku moja tu,
16
mtu wa kwenu akawaambia: Nendeni na kutengemana, mwote moto, mpate kushiba! asiwape yaipasayo miili yao, itawafaliaje?
17
Hapo mwaona: Kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo yakupasayo kumekwisha kuangamika kwenyewe.*
18
Labda yuko atakayesema: Wewe uko na kumtegemea Mungu, nami niko na matendo; nionyesha, unavyomtegemea Mungu pasipo matendo! kisha nami nitakuonyesha, matendo yangu yanavyotimilika katika kumtegemea Mungu.
19
Wewe unaamini, ya kuwa Mungu ni mmoja tu? Ni vizuri; pepo nao huyaamini hayo, lakini hutetemeka!
20
Mtu mpuzi, unataka kutambua, ya kuwa kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo ni kwa bure?
21
Baba yetu Aburahamu hakupata wongofu kwa matendo alipompeleka mwana wake Isaka, awe ng'ombe ya tambiko?
22
Unaona: Kumtegemea Mungu husaidiana na matendo yakupasayo; napo, alipofanya yampasayo, ndipo, kumtegemea Mungu kulipotimilika kwake,
23
nayo yaliyoandikwa yakatimia kwamba: Aburahamu alimtegemea Mungu, kwa hiyo akawaziwa kuwa mwenye wongofu, akaitwa mpenzi wake Mungu.
24
Mnaona: Mtu hupata wongofu kwa matendo, siko kwa kumtegemea Mungu tu.
25
Tena je? Yule mke mgoni Rahabu hakupata wongofu naye kwa matendo, alipowafikiza wale wajumbe na kuwatoa mjini kwa njia nyingine?
26
Kwani kama mwili unavyokufa, usipopumua, vivyo hivyo nako kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo kunakufa.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5