bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
James 3
James 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 4 →
1
Ndugu zangu, haifai, wengi wakiwa wafunzi. Jueni: hukumu, tutakayoipata sisi, itakuwa kuliko ya wengine!
2
Kwani sisi sote hukosa mengi. Mtu asipokosa kwa kusema, huyo ni mume mtimilifu anayeweza kuuongoza hata mwili wote.
3
Tazameni, farasi twawatia hatamu vinywani, watutii sisi; nasi hivyo huwaongoza miili yao yote kwenda huko, tunakopenda.
4
Tazameni, hata merikebu zilivyo kubwa sana, tena zinavyochukuliwa na pepo zenye nguvu! Nazo huongozwa na sukani iliyo ndogo sana, mwenye kuishika anakotaka.
5
Vivyo hivyo nao ulimi ni kiungo kidogo, nao hujivunia makuu! Tazameni, moto ulio mdogo huchoma pori kubwa!
6
Nao ulimi ni moto, ni ulimwengu wenye upotovu. Katika viungo vyetu ndio ulimi unaouchafua mwili wote, unavichoma vyote vilivyoumbwa, wenyewe ukiwashwa na moto ulioko kuzimuni.
7
Kwani nyama wo wote, kama nyama wa porini na ndege na nyoka na nyama wa baharini, wote hufugika, nao wamekwisha fugwa na nguvu za watu.
8
Lakini huo ulimi hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu yenye kuua.
9
Ndio, unaotutukuzisha Bwana aliye Baba, tena ndio, unaotuapizisha watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
10
Matukuzo na maapizo hutoka katika kinywa kilekile kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapasi kuwa hivyo.
11
Je? Iko chemchemi inayotoa maji matamu na machungu katika kisima kilekile kimoja?
12
Ndugu zangu, uko mkuyu unaoweza kuzaa chikichi, au mzabibu unaoweza kuzaa kuyu? Napo penye chumvi hapatoki maji matamu.
13
Kwenu yuko nani aliye mwerevu wa kweli wa kujua mambo? Ajionyeshe kuwa mwenye mwenendo mzuri, nazo kazi zake zijulike kuwa zenye upole utokao katika huo werevu wa kweli!
14
Lakini mkiwa wenye wivu ulio na uchungu na wenye uchokozi mioyoni mwenu msijivune, wala yaliyo ya kweli msiyageuze kuwa uwongo!
15
Kwani werevu huu haukutoka mbinguni juu, ila nchini, ni wa kimtu na wa Kisatani.
16
Kwani wivu na uchokozi ulipo, ndipo palipo penye matata na mambo maovu yo yote.
17
Lakini werevu wa kweli utokao mbinguni juu kwanza ni wenye ung'avu, kisha ni wenye utengemano na upole na unyenyekevu, huwahurumia wote na kuwapatia mazao mema; haupendelei, maana hukataa ujanja.
18
Nalo tunda la kuzaa wongofu hupandwa nao wenye utengemano panapotengemana.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5