bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Lamentations 1
Lamentations 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
1
Kumbe uliokuwa mji wenye watu wengi unakaa peke yake! Uliokuwa mkuu katika wamizimu ukawa kama mjane! Uliokuwa mfalme wa kike wa miji unatumikishwa!
2
Unalia usiku kucha, machozi yake yako mashavuni pake! Hakuna autulizaye moyo kwao wote walioupenda, wenziwe wote wakauacha kwa udanganyifu, wakawa adui zake.
3
Wayuda wametekwa, wakapatwa na wasiwasi na utumishi mwingi; wanakaa kwenye wamizimu pasipo kuona kituo, wote waliowakimbiza wakawapatia mahali pa kubanana.
4
Njia za Sioni zinasikitika, kwani hakuna wajao kula sikukuu, malango yake yote yako peke yao, watambikaji wake wanapiga kite, wanawali wake wametiwa majonzi, nao wanayaona kuwa machungu.
5
Wausongao wako juu, adui zake wanafanikiwa, kwani Bwana ameutia majonzi kwa ajili ya mapotovu yake mengi, wachanga wake wakatekwa na kuhamishwa mbele yao wawasongao.
6
Utukufu wake wote umemtoka yeye binti Sioni, wakuu wake wakawa kama kulungu wasioona malisho, wakaenda pasipo nguvu mbele yao wawakimbizao.
7
Siku hizi za ukiwa na za kutangatanga Yerusalemu unayakumbuka mema yake yote yaliyoupendeza, ambayo ulikuwa nayo siku za kale. Watu wake walipotiwa mkononi mwake aliyewasonga, mwenye kuwasaidia hakuwako kabisa; waliowasonga walipoviona, wakacheka, jinsi walivyokomeshwa
8
Yerusalemu umekosa kweli, kwa hiyo ukawa tapisho, wote walioutukuza wakaubeza, kwani waliuona, ulipokuwa uchi, nao unapiga kite kwa kurudi nyuma.
9
Uchafu wake umezishika nguo zake ndefu, haukukumbuka mwisho kama huu; hivyo ulivyobwagwa chini unastaajaabisha, tena hakuna anayeutuliza moyo. E Bwana, utazame ukiwa wangu! Kwani adui wanajikuza.
10
Mwenye kuusonga ameukunjua mkono wake, ayachukue mema yake yote yapendezayo; kwani aliona wamizimu, wakipaingia Patakatifu pake, nawe uliwakataza, wasipaingie penye mkutano wako!
11
Watu wake wote wanapiga kite wakitafuta chakula, mema yao yapendezayo wanayanunua vilaji vya kujirudisha uzimani. Tazama, Bwana, uone, ya kuwa ninawaziwa kuwa si kitu!
12
Je? Ninyi nyote mpitao njia, haviingii mioyoni mwenu? Chungulieni, mwone, kama yako maumivu yaliyo sawa nayo yangu yaliyonipata mimi, maana nimetiwa majonzi na Bwana, makali yalipomwaka moto.
13
Toka juu akatuma moto kuiingia mifupa yangu, nao ukaishinda; miguu yangu akaitegea tanzi, akanirudisha nyuma, akanipa kuwa peke yangu, kwa hiyo ninaugua mchana kutwa.
14
Mzigo wa mapotovu yangu ukafungwa kwa mkono wake, yaliposhikamana yakawekwa shingoni pangu; ndivyo, alivyozivunja nguvu zangu. Bwana akanitia mikononi mwao, ambao siwezi kuwainukia.
15
Wanguvu wangu Bwana akawatupa wote, waondoke kwangu; akaita wengi, wanikusanyikie wawaponde wavulana wangu, mwanamwali binti Yuda Bwana akamkanyaga kamulioni.
16
Kwa hiyo ninalia machozi, macho yangu mawili hutiririka maji, kwani mtuza moyo anikalia mbali, ndiye awezaye kuirudisha roho yangu. Watoto wangu wameachwa peke yao, kwani adui wanazidi nguvu.
17
Sioni unainyosha mikono yake, lakini hakuna anayeutuliza moyo Bwana amewaagiza wamzungukao Yakobo, wamsonge tu; ndipo, Yerusalemu ulipowaziwa kwao kuwa si kitu.
18
Lakini Bwana ni mwongofu, kwani nalikiinukia kinywa chake. Yasikieni, ninyi makabila yote, kayatazameni maumivu yangu! Wavulana na wasichana wangu wametekwa na kuhamishwa!
19
Nikawaita walionipenda, lakini wakanidanganya. Watambikaji na wazee wangu wamezimia mijini walipojitafutia vyakula, wazirudishe roho zao.
20
Tazama, Bwana! Kwani nimesongeka: matumbo yangu yamechafuka, moyo wangu nao humu kifuani umepinduliwa, kwa kuwa nalikataa kukutii kabisa. Nje upanga unawaua watoto, nyumbani huwa kama mwake kifo.
21
Wakasikia, nilivyougua, lakini hakuna anitulizaye moyo, adui zangu wote walipoyasikia mabaya yaliyonipata, wakayafurahia, ya kuwa ndiyo, uliyoyafanya wewe. Utaileta ile siku, uliyoitangaza, ndipo, watakapokuwa kama mimi.
22
Mabaya yao yote na yatokee usoni pako, uwafanyizie, kama ulivyonifanyizia kwa ajili ya mapotovu yangu yote! Kwani kupiga kite kwangu ni kwingi, nao moyo wangu huugua tu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5