bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Lamentations 4
Lamentations 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
1
Imekuwaje, dhahabu ikichujuka, dhahabu iliyo nzuri yenyewe ikigeuka kuwa mbaya? Imekuwaje, vijiwe vya pambo vya Patakatifu vikitupwa pembeni penye barabara zote?
2
Vijana wa Sioni waliohesabiwa kuwa mali, waliolinganishwa na dhahabu tupu, imekuwaje, wakiwaziwa kuwa vyombo vya udongo vinavyofanywa kwa mikono ya mfinyanzi?
3
Mbwa wa mwitu nao hutoa maziwa ya kuwanyonyesha watoto wao, lakini wanawake wao walio ukoo wangu wamegeuka, wasione uchungu kama mbuni wa nyikani.
4
Ndimi za vitoto vinyonyavyo zinagandamana na fizi zao kwa kiu; wana wachanga wanaomba mkate, lakini hakuna anayewamegea.
5
Waliokula vya urembo wanazimia barabarani kwa njaa, waliokuzwa na kuvikwa mavazi mororo ya kifalme sasa wanalala jaani.
6
Manza, walizozikora wazaliwa wa ukoo wangu, ni kubwa kuliko makosa ya Sodomu uliogeuzwa kwa kitambo kimoja kuwa si mji tena, lakini haikuwako mikono ya watu iliyougusa tu.
7
Wakuu wao waling'aa kuliko theluji, wakawa weupe kuliko maziwa; miili yao ilikuwa miekundu kuliko marijani, sura zao zilikuwa kama za jiwe la safiro;
8
lakini sasa ukiwatazama, ni weusi kuliko masizi, hawajulikani barabarani, ngozi zao zimekunjana na kugandamana na mifupa yao, zimekauka, zikawa kama maganda ya mti.
9
Waliouawa kwa panga ndio waliopata mema, kuliko wao waliouawa kwa njaa; hao ndio waliozimia wakichomwa na ukosefu wa mazao ya mashamba.
10
Ikawa, wanawake wenye uchungu wakawatokosa wana wao wenyewe kwa mikono yao, wawe chakula chao hapo, wazaliwa wa ukoo wangu walipovunjwa.
11
Bwana ameyatimiza machafuko yake, akayamwaga makali yake yenye moto; hivyo ndivyo, alivyowasha moto Sioni ulioila nayo misingi yake.
12
Wafalme wa nchi nao wote wakaao humu ulimwenguni kwao hakuwako aliyeitikia kwamba: Malangoni mwa Yerusalemu ataingia ausongaye au adui ye yote.
13
Hayo yamefanyika kwa ajili ya makosa ya wafumbuaji wake na kwa ajili ya maovu, watambikaji waliyoyafanya walipomwaga mwake katikati damu zao waliokuwa waongofu.
14
Wakatangatanga barabarani kama vipofu, kwa kuwa walijichafua kwa damu, watu wasiweze kabisa kuzigusa nguo zao.
15
Mwondokeeni mchafu! Ndivyo, watu walivyotangaza mbele yao. Ondokeni! Ondokeni! Msiwaguse! Walipopiga mbio na kutangatanga hivyo, watu wakasema nako kwa wamizimu: Wasikae tena kuwa wageni wetu!
16
Macho ya Bwana yenye ukali yakawatenga, naye hatawatazama tena; kwani hawakuwaheshimu watambikaji, wala wazee hawakuwahurumia.
17
Nasi macho yetu yakafifia yasipokoma kuutazamia msaada wetu, lakini haukupatikana; katika kilindo chetu tukaendelea kuchungulia taifa, lakini halikuwako lililoweza kutuokoa.
18
Wakazinyatia nyayo zetu, tusiweze kwenda katika barabara zetu; mwisho wetu uko karibu, siku zetu zimetimia, kwani mwisho wetu umefika.
19
Watukimbizao ni wepesi kuliko tai wa mbinguni, wakatufukuza nako milimani juu na kutuvizia nyikani.
20
Aliyekuwa kama pumzi puani mwetu yeye aliyepakwa mafuta na Bwana akanaswa katika mashimo yao; ni yeye, tuliyemsema: Kivulini kwake tutakaa kwenye makabila ya watu
21
Furahi na kujichekelea, binti Edomu, ukaaye katika nchi ya Usi! Wewe nawe kitakufikia hiki kinyweo, ulewe, mpaka ujikalishe mwenye uchi.
22
Manza, ulizozikora, binti Sioni, zimemalizika: Bwana hatakutoa tena, uhamishwe. Manza, ulizozikora, binti Edomu, atakupatilizia atakapoyavumbua makosa yako.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5