bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Lamentations 2
Lamentations 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 3 →
1
Kumbe Bwana kwa makali yake anamkalisha binti Sioni chini! Utukufu wa Isiraeli uliofika hata mbinguni ameubwaga chini, alipokasirika hakukumbuka, ya kuwa ni pake pa kuiwekea miguu yake.
2
Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo pasipo kuyaonea uchungu, kwa machafuko yake akayabomoa maboma ya binti Yuda, mfalme nao wakuu wake akawakumba, waanguke, kisha akawachafua.
3
Makali yake yalipowaka moto, ndipo, alipokata pembe zote za Isiraeli, akaurudisha nyuma mkono wake wa kuume, uondoke usoni pa adui, akachoma moto kwake Yakobo, ukawa wenye miali iliyokula po pote.
4
Akaupinda upindi wake, akawa kama adui, akajipanga na kuutumia mkono wake wa kuume, kama mwenye kusonga, akawaua wote walipendeza macho; hemani mwake binti Sioni ndimo, alimoyaeneza makali yake kama moto.
5
Bwana akawa kama adui, alipommeza Isiraeli, akayameza majumba yake, akayaangamiza maboma yake, akamfurikishia binti Yuda kupiga kite na kuugua.
6
Akakivunja kitalu chake kama cha bustanini, akauangamiza ua wake uliokuwa wa kukusanyikia; kisha Bwana akawasahaulisha Wasioni sikukuu nazo za mapumziko, akamtupa mfalame na mtambikaji, makali yake yalipowapatiliza.
7
Pake pa kutambikiwa Bwana akapaona kuwa pabaya, napo Patakatifu pake, akapaacha. Akazitia mikononi mwa adui kuta za majumba yake, wakapiga makelele Nyumbani mwa Bwana kama yale ya sikukuu.
8
Bwana amewaza moyoni kuziangamiza kuta za binti Sioni, akapapitisha kamba ya kupimia, hakuurudisha mkono, usipatoweshe, akalisikitisha boma pamoja na kuta zake, sasa zinatia uchungu.
9
Malango yake yamezama, yamo mchangani ndani, makomeo yake akayaharibu kwa kuyavunja. Mfalme wake pamoja na wakuu wako kwa wamizimu, huko hawasikii, Maonyo yakisomwa, wala wafumbuaji wake hawafumbuliwi maono naye Bwana.
10
Wazee wake binti Sioni hukaa chini na kunyamaza kimya, hujitupia mavumbi vichwani na kujifunga magunia, wanawali wa Yerusalemu huvielekeza vichwa vyao chini.
11
Macho yangu yamezimia kwa kulia machozi, matumbo yangu nayo huchafuka; maini yangu yamemwagika chini kwa ajili ya mavunjiko yao walio wazaliwa wa ukoo wangu, kwani wachanga na wanyonyaji huzimia roho barabarani mjini.
12
Nao huwauliza mama zao: Mikate na mvinyo iko wapi? wanapozimia barabarani mjini kama wenye kupigwa kwa panga, au wanapokata roho vifuani kwa mama zao.
13
Nikutolee ushuhuda gani? Nikufananishe na nini, binti Yerusalemu? Nikulinganishe na nini, nikutulize moyo, mwanamwali binti Sioni? Kwani vunjiko lako ni kubwa kama bahari, atakayekuponya ni nani?
14
Wafumbuaji wako waliyoyaona yalikuwa uwongo na upumbavu, hawakuyafunua maovu yako, uliyoyafanya, wayafungue mafungo yako, ila walipokuambia: Tumeona, yalikuwa uwongo, wakupatie kutekwa.
15
Wote wapitao njiani wanakupigia makofi, hukuzomea, binti Yerusalemu, wakivitingisha vichwa vyao, kwamba: Je? Huu ni ule mji, watu waliouita: Timilizo la uzuri, tena: Furaha ya nchi zote?
16
Adui zako wote wakaviasama vinywa vyao, wakakuzomea wakikukerezea meno na kusema: Tumemmeza! Hii ni siku, tuliyoingojea, tumeipata, tumeiona!
17
Bwana ameyafanya aliyoyawaza, akalitimiza neno lake, aliliagiza tangu siku za kale, akabomoa pasipo kuona uchungu, adui zako wakakufurahia, alipozikuza pembe zao waliokusonga
18
Mioyo yao ikamlilia Bwana: Ninyi kuta za binti Sioni, churuzisheni machozi mchana na usiku kama ni mto! Usijipatie pumziko! Mboni ya jicho lako isinyamaze!
19
Inuka, ulie usiku kucha, zamu za usiku zikipokeana! Umwage moyo wako, kama ni maji mbele ya uso wake Bwana! Mnyoshee mikono yako kwa ajili ya roho za watoto wako wachanga wanaozimia kwa njaa po pote barabarani pembeni!
20
E Bwana, tazama, uone! Ni nani, uliyemfanyizia hivyo? Je? Wanawake wayale mazao yao, watoto wao waliolelewa nao? Je? Watambikaji na wafumbuaji wauawe Patakatifu pake Bwana?
21
Wana wa wazee hulala barabarani chini, wasichana na wavulana wangu wameuawa kwa panga; umewaua siku ile, makali yako yalipotokea, ukawachinja pande zote pasipo kuwaonea uchungu!
22
Ukawaita wote walionitia woga, watoke pande zote, kama ni siku ya mkutano, lakini ilikuwa siku ya makali ya Bwana, napo hapo hawakuwako walioona pa kuponea wala pa kukimbilia, nao, niliowalea na kuwakuza, adui wakawamaliza.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5