bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Lamentations 5
Lamentations 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
1
Bwana, yakumbuke yaliyotupata! Tazama, uone, jinsi tunavyotiwa soni!
2
Mafungu yetu ya nchi yamechukuliwa, yawe mali za wengine, nyumba zetu zinakaa wageni.
3
Tumegeuka kuwa wana waliofiwa na baba zao, mama zetu ni kama wajane.
4
Maji yetu tunayanywa tukiyanunua kwa fedha, kuni zetu nazo tunazipata tu tukizilipa.
5
Watukimbizao wako penye shingo zetu; tunapochoka hatuoni pa kupumzika.
6
Wamisri na Waasuri tukawanyoshea mikono, tupate vyakula vya kushiba.
7
Baba zetu waliokosa hawako tena, nasi tunatwikwa manza, walizozikora wao.
8
Watumwa ndio wanaotutawala, lakini hakuna anayetupokonya mikononi mwao.
9
Tunaziponza roho zetu tukijichumia vyakula, kwa kuwa nako nyikani ziko panga.
10
Ngozi zetu ni zenye moto kama wa tanuru kwa kuteketezwa na njaa.
11
Wanawake waliokuwamo Sioni waliwakorofisha, nao wasichana waliokuwako katika nchi za Yuda.
12
Wakuu wakanyongwa kwa mikono yao, nazo nyuso za wazee hazikupewa macheo.
13
Vijana hutwikwa majiwe ya kusagia, watoto huvunjwa na mizigo ya kuni.
14
Ndipo, wazee walipoyaacha maongezi ya malangoni, nao vijana wakayakomesha mazeze yao.
15
Yakakoma yaliyoifurahisha mioyo yetu, michezo yetu ya ngoma ikageuka kuwa maombolezo.
16
Vilemba vilivyovipamba vichwa vyetu vimekwisha kuanguka chini, tukapatwa na mabaya, kwa kuwa tumekosa.
17
Kwa hiyo mioyo yetu imezimia, kwa hiyo macho yetu nayo yameguiwa na giza.
18
Ni kwa ajili ya mlima wa Sioni ulioko peke yake, kwa kuwa ni mbweha tu wanaotembea huko.
19
Wewe Bwana, unakaa kale na kale, kiti chako cha kifalme kiko kwa vizazi na vizazi!
20
Mbona unatusahau kale na kale, ukatuacha siku hizi zilizo nyingi?
21
Bwana, turudishe kwako! Ndivyo, tutakavyopata kurudi; siku zetu zigeuke kuwa mpya tena kama zile zilizopita!
22
Kweli umetutupa kabisa, umetukasirikia sanasana.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
All chapters:
1
2
3
4
5