bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Lamentations 3
Lamentations 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 4 →
1
Mimi ni mtu wa kiume, lakini niliteseka nilipopigwa fimbo yenye machafuko yake.
2
Akaniongoza na kuniendesha, nije gizani, nisije mwangani.
3
Ananirudia mimi peke yangu, mkono wake ukinigeukia mchana kutwa.
4
Akazinyausha nyama na ngozi za mwili wangu mimi, mifupa yangu yote akaivunja nayo.
5
Akanizibia njia akanizungushia mambo yenye sumu na usumbufu.
6
Akanikalisha penye giza kuu kama waliokufa kale.
7
Ukuta unanizunguka, nisitoke, akanifunga minyororo mizito.
8
Ijapo nilie na kupiga yowe, maombo yangu huyazibia masikio.
9
Akazifunga njia zangu kwa mawe yaliyochongwa, napo pengine, nilipopita, akapafanya, pasipitike tena.
10
Yeye akaniwia kama nyegere aoteaye au kama simba aliomo mafichoni.
11
Njia zangu akazipoteza, akaninyafua, akaniweka mahali palipo peke yake.
12
Akaupinda upindi wake, akanitumia kuwa shabaha ya kuipiga mishale.
13
Iliyokuwa podoni mwake akaipiga, inichome mafigo
14
Nikawa kicheko kwao wote walio ukoo wangu, wakanizomea mchana kutwa.
15
Akanishibisha kwa kunilisha yaumizayo matumbo, akaninywesha maji machungu.
16
Akayakerezesha meno yangu na kuyaumisha vijiwe, akanigaagaza majivuni.
17
Ukaifukuza roho yangu, isipate kutulia, nikasahau kulivyo, mtu akikaa vema.
18
Nikasema: Nguvu zangu zimepotea pamoja na kingojeo changu cha kumngojea Bwana.
19
Ukumbuke ukiwa wangu na wasiwasi wangu, nikilishwa machungu, nikinyweshwa yenye sumu!
20
Roho yangu haiachi kuyakumbuka, kwa kuwa imeinamishwa humu ndani yangu.
21
Haya na niyaweke moyoni tena, ndivyo, nitakavyopata kumngojea:
22
*Ni upole wake Bwana, tusipomalizika, kwani huruma zake hazikuisha,
23
kila kunapokucha ni mpaya, nao walekevu wake ni mwingi.
24
Fungu langu ni Bwana! ndivyo, roho yangu isemavyo: kwa hiyo nitamngojea.
25
Bwana huwawia mwema wamngojeao nao wamtafutao kwa roho.
26
Inafaa kuvumilia na kuungojea wokovu wa Bwana.
27
inamfalia mtu wa kiume, akitwikwa mizigo akingali kijana bado.
28
Na akae peke yake na kunyamaza kimya, kwani Bwana ndiye aliyemtwika.
29
kinywa chake akiweke uvumbini, kwani labda liko la kulingojea.
30
Ampigaye na amgeuzie shavu, na ashibe matusi.
31
Bwana hamtupi mtu kale na kale.
32
Bwana akimtia mtu majonzi atamhurumia tena, kwani upole wake ni mwingi.*
33
Kwani siko kupenda kwa moyo wake, akiwaumiza wana wa watu na kuwapiga.
34
Mtu akiwaponda na kuwapiga mateke kwa miguu wote waliofungwa huku nchini,
35
au mtu akimpotoa mwenziwe na kumnyima yampasayo usoni pake Alioko huko juu,
36
au mtu akimgeuza mwenziwe mkweli shaurini kuwa mwongo, Bwana asiyatazame?
37
Yuko nani awezaye kusema neno, likawapo, Bwana asipoliagiza?
38
Je? Yeye Alioko huko juu aliyoyasema, hayatokei yakiwa mabaya au yakiwa mema?
39
Mtu hununia nini siku zote za kuwapo? Kila mtu na ayanunie makosa yake!
40
Na tuzijaribu njia zetu na kuzichunguza, tupate kurudi upande wake Bwana!
41
Na tumwinulie Mungu mbinguni mioyo yetu pamoja na mikono yetu!
42
Sisi ndio tuliokosa tusipokutii, nawe hukutuondolea.
43
Ulipojivika makali ulitukimbiza, ukaua pasipo huruma.
44
Ukajivika wingu, likufunike, malalamiko yasikufikie.
45
Ukatufanya kuwa takataka za kutupwa tu katikati ya makabila ya watu.
46
Wakatuasamia vinywa vyao wote waliokuwa adui zetu.
47
Yaliyotupata yalikuwa mastuko na mashimo na maangamizo na mavunjiko.
48
Macho yangu huchuruzika vijito vya maji kwa ajili ya mavunjiko yao walio wazaliwa wa ukoo wangu.
49
Macho yangu hulia machozi pasipo kupumzika, hayakomeki,
50
mpaka Bwana achungulie toka mbinguni, ayaone.
51
Macho yangu huniumiza roho kwa kuona, wanawake wote wa mji wangu walivyo.
52
Kweli wameniwinda kama ndege wale wanichukiao bure tu;
53
wakanitupa shimoni, wanizimishe roho, wakanitupia mawe.
54
Maji yenye nguvu yakakididimiza kichwa changu, nikasema: Basi, nimekatwa roho.
55
nikalililia Jina lako, Bwana, nilipokuwa shimoni kuzimuni.
56
Ukaisikia sauti yangu nilipokuomba: Usiyazibe masikio yako, nikikupigia kite na kukuomba wokovu.
57
Ukanijia karibu siku ile, nilipokulilia, ukaniambia: Usiogope!
58
Ukanigombea magomvi ya roho yangu ukanikomboa na kunirudisha uzimani.
59
Ukaona, Bwana, jinsi nilivyopotolewa, ukayakata mashauri yangu.
60
Ukayaona yote, waliyoyataka kunilipizia, nayo yote, waliyoyawaza ya kunifanyizia.
61
Ukayasikia, Bwana, matusi yao nayo yote, waliyoniwazia.
62
Ukayasikia, waniinukiao waliyoyasema wakinipigia mashauri mchana kutwa.
63
Tazama, uone! Ikiwa wanakaa, au ikiwa wanasimama: mimi ndiye, wanayemzomea.
64
Uwalipishe, Bwana, matendo yao ukiwafanyizia, kama mikono yao ilivyofanya!
65
Uwashupaze mioyo yao, apizo lako likiwajia!
66
Uwakimbize kwa makali yako na kuwaangamiza, watoweke chini ya mbingu za Bwana!
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5