bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Job 12
Job 12
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 13 →
1
Ndipo Ayubu akajibu:
2
“Bila shaka ninyi ndio watu, nayo hekima itakoma mtakapokufa!
3
Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi; mimi si duni kwenu. Ni nani asiyejua mambo haya yote?
4
“Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu, ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu: mimi ni mtu wa kuchekwa tu, ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia!
5
Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza.
6
Mahema ya wanyang’anyi hayasumbuliwi, wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama: wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao.
7
“Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, au ndege wa angani, nao watawaambia;
8
au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, au acheni samaki wa baharini wawape taarifa.
9
Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua kwamba mkono wa Mwenyezi Mungu ndio uliofanya hili?
10
Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe, na pumzi ya wanadamu wote.
11
Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula?
12
Je, hekima haipatikani kwa wazee? Je, maisha marefu hayaleti ufahamu?
13
“Hekima na nguvu ni vya Mungu; shauri na ufahamu ni vyake yeye.
14
Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.
15
Akizuia maji, huwa pana ukame; akiyaachia maji, huharibu nchi.
16
Kwake kuna nguvu na ushindi; anayedanganywa na anayedanganya, wote wawili ni wake.
17
Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.
18
Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, na kuwafunga mishipi ya kiunoni.
19
Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.
20
Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, na kuondoa busara ya wazee.
21
Huwadharau wanaoheshimika, na kuwavua silaha wenye nguvu.
22
Hufunua mambo ya ndani ya gizani, na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.
23
Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya.
24
Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao; huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia.
25
Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga; huwafanya wapepesuke kama walevi.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42