bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Job 36
Job 36
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 37 →
1
Elihu akaendelea kusema:
2
“Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonesha kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu.
3
Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu.
4
Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe.
5
“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika kusudi lake.
6
Hawaachi waovu waendelee kuishi, bali huwapa walioteswa haki yao.
7
Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; huwaketisha penye viti vya utawala pamoja na wafalme, na kuwatukuza milele.
8
Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,
9
huwaonesha yale waliyoyatenda, kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.
10
Huwafanya wao kusikia maonyo, na huwaagiza kutubu uovu wao.
11
Wakitii na kumtumikia, wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, na miaka yao katika utoshelevu.
12
Lakini wasiposikiliza, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa.
13
“Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; hata anapowafunga, hawamwombi msaada.
14
Wanakufa wangali vijana, miongoni mwa mahanithi wa mahali pa ibada za sanamu.
15
Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao, na kuzungumza nao katika dhiki zao.
16
“Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki, ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi, hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri.
17
Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu; hukumu na haki vimekukamata.
18
Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri; usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa.
19
Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki?
20
Usiutamani usiku uje, ili uwaburute watu mbali na nyumba zao.
21
Jihadhari usigeukie uovu, ambao unaupenda zaidi ya mateso.
22
“Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. Ni nani aliye mwalimu kama yeye?
23
Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’?
24
Kumbuka kuzitukuza kazi zake, ambazo watu wamezisifu katika wimbo.
25
Wanadamu wote wameiona; watu wanaikazia macho kwa mbali.
26
Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27
“Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka vijito;
28
mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.
29
Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, jinsi angurumavyo kutoka kwenye hema lake.
30
Tazama anavyotandaza radi yake kumzunguka, naye huvifunika vilindi vya bahari.
31
Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, na kuwapa chakula kwa wingi.
32
Huujaza mkono wake kwa radi, na kuiagiza kulenga shabaha yake.
33
Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja; hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 37 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42