bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Job 20
Job 20
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 21 →
1
Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu:
2
“Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu, kwa sababu nimehangaika sana.
3
Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima, nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu.
4
“Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani, tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani,
5
macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.
6
Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni na kichwa chake hugusa mawingu,
7
ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe. Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’
8
Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.
9
Jicho lililomwona halitamwona tena; mahali pake hapatamwona tena.
10
Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyang’anya watu.
11
Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, zitalala naye mavumbini.
12
“Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake,
13
ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, lakini huuweka kinywani mwake.
14
Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.
15
Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.
16
Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.
17
Hatafurahia vijito, mito inayotiririsha asali na siagi.
18
Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.
19
Kwa kuwa aliwadhulumu maskini na kuwaacha bila kitu; amenyang’anya kwa nguvu nyumba asizozijenga.
20
“Hakika hatakuwa na amani katika kutamani kwake; hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.
21
Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale; kufanikiwa kwake hakutadumu.
22
Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; taabu itamjia kwa nguvu zote.
23
Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake.
24
Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, mshale wa shaba utamchoma.
25
Atauchomoa katika mgongo wake, ncha inayong’aa kutoka ini lake. Vitisho vitakuja juu yake;
26
giza nene linavizia hazina zake. Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.
27
Mbingu zitaweka wazi hatia yake, nayo nchi itainuka kinyume chake.
28
Mafuriko yataichukua nyumba yake, maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.
29
Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu, urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42