bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Job 30
Job 30
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 31 →
1
“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuliko mimi wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.
2
Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia?
3
Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa, walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa.
4
Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi, nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio.
5
Walifukuzwa mbali na watu wao, wakipigiwa kelele kama wezi.
6
Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka, kwenye majabali na mahandaki.
7
Kwenye vichaka walilia kama punda, na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka.
8
Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya, waliofukuzwa watoke katika nchi.
9
“Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo; nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.
10
Wananichukia sana na kujitenga nami, wala hawasiti kunitemea mate usoni.
11
Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa, wamekuwa huru kunitendea wanavyopenda.
12
Kuume kwangu kundi linashambulia; wao huitegea miguu yangu tanzi, na kunizingira.
13
Huizuia njia yangu, nao hufanikiwa katika kuniletea maafa, nami sina yeyote wa kunisaidia.
14
Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana; katikati ya magofu huja na kunishambulia.
15
Vitisho vimenifunika; heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo, salama yangu imetoweka kama wingu.
16
“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; siku za mateso zimenikamata.
17
Usiku mifupa yangu inachoma; maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe.
18
Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo; hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu.
19
Yeye amenitupa kwenye matope, nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20
“Ee Mwenyezi Mungu, ninakulilia wewe lakini hunijibu; ninasimama, nawe unanitazama tu.
21
Wewe unanigeukia bila huruma; unanishambulia kwa nguvu za mkono wako.
22
Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; umenirusharusha kwenye dhoruba.
23
Ninajua utanileta hadi kifoni, mahali wenye uhai wote wamewekewa.
24
“Hakika hakuna mtu anayemshambulia mhitaji anapoomba msaada katika shida yake.
25
Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini?
26
Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.
27
Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili.
28
Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada.
29
Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.
30
Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika; mifupa yangu inaungua kwa homa.
31
Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo, nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42