bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Kings 12
1 Kings 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 13 →
1
Rehabeamu akaenda Sikemu, kwani Waisiraeli wote walifika Sikemu kumpa ufalme.
2
Naye Yeroboamu, mwana wa Nebati, akayasikia, lakini alikuwa angaliko huko Misri, alikokimbilia alipomkimbia mfalme Salomo; huko Misri ndiko, Yeroboamu alikokaa.
3
Walipotuma kumwita, Yeroboamu akaja na mkutano wote wa Waisiraeli, wakamwambia Rehabeamu kwamba:
4
Baba yako alitutwisha mzigo mzito, nawe wewe sasa utupunguzie ule utumwa mgumu wa baba yako nao mzigo wake mzito, aliotutwisha! Kisha tutakutumikia.
5
Akawaambia: Nendeni kwanza siku tatu, kisha rudini kwangu! Watu walipokwenda zao,
6
mfalme Rehabeamu akafanya shauri na wazee waliomtumikia baba yake Salomo, alipokuwa mzima bado, akawauliza: Ninyi shauri lenu ni nini? Watu hawa tuwape majibu gani?
7
Wakamwambia hivi: Ukiwaitikia leo watu hawa na kuwatumikia, tena ukiwajibu na kuwaambia maneno mema, ndipo, watakapokuwa watumishi wako siku zote.
8
Lakini akaliacha shauri la wazee, walilompa, akafanya shauri na vijana waliokua naye na kumtumikia,
9
akawauliza: Ninyi shauri lenu ni nini? tuwape majibu gani watu hawa walioniambia: Tupunguzie mzigo, aliotutwisha baba yako?
10
Vijana hawa waliokua naye wakasemezana naye kwamba: Haya ndiyo, uwaambie watu hao waliokuambia kwamba: Baba yako aliukuza mzigo wetu kuwa mzito, wewe utupuzie huo mzigo wetu, basi uwaambie hivyo: Kidole changu kidogo na kinenepe kuliko viuno vya baba yangu,
11
sasa vitakuwa hivi: kama baba yangu aliwatwisha mzigo mzito, mimi nitauzidisha mzigo wenu; kama baba yangu aliwapiga fimbo, mimi nitawapiga viboko vyenye miiba.
12
Yeroboamu na watu wote wakaja kwake Rehabeamu siku ya tatu, kama mfalme alivyosema kwamba: Rudini kwangu siku ya tatu!
13
Ndipo, mfalme alipowapa hawa watu majibu magumu akiliacha shauri la wazee, walilompa,
14
akasema nao na kulifuata shauri la vijana kwamba: Kama baba yangu aliwatwisha mzigo mzito, mimi nitauzidisha; kama baba yangu aliwapiga fimbo, mimi nitawapiga viboko vyenye miiba.
15
Mfalme hakuwasikia wale watu, kwani Bwana aliyageuza kuwa hivyo, apate kulitimiza neno lake, alilomwambia Yeroboamu, mwana wa Nebati, kinywani mwa Ahia wa Silo.
16
Waisiraeli wote walipoona, ya kuwa mfalme hakuwasikia, ndipo, watu walipomjibu mfalme neno la kwamba: Sisi tuna bia gani na Dawidi? Hatuna fungu lo lote kwake mwana wa Isai. Waisiraeli, haya! Rudini sasa mahemani kwenu! Nawe Dawidi, na uuangalie mwenyewe mlango wako! Ndipo, Waisiraeli walipokwenda mahemani kwao.
17
Ni wana wa Isiraeli waliokaa katika miji ya Yuda tu, Rehabeamu aliowapata, awe mfalme wao.
18
Mfalme Rehabeamu alipomtuma Adoramu aliyekuwa msimamizi wa kazi za nguvu, wana wa Isiraeli wote wakampiga mawe, hata akafa. Kisha mfalme Rehabeamu akajihimiza kupanda garini na kukimbilia Yerusalemu.
19
Ndivyo, Waisiraeli walivyojitenga na mlango wa Dawidi mpaka siku ya leo.
20
Ikawa, Waisiraeli wote waliposikia, ya kuwa Yeroboamu amerudi, wakatuma kumwita kuja kwenya mkutano, wakamfanya kuwa mfalme wa Waisiraeli wote, hakuna aliyeufuata mlango wa Dawidi, ni shina la Yuda peke yake tu.
21
Rehabeamu alipofika Yerusalemu akaukusanya mlango wote wa Yuda na shina la Benyamini, watu 180000 waliochaguliwa kupiga vita, wapigane na mlango wa Waisiraeli, wamrudishie Rehabeamu, mwana wa Salomo, ufalme huo.
22
Lakini neno la Mungu likamjia Semaya aliyekuwa mtu wa Mungu, kwamba:
23
Mwambie Rehabeamu, mwana wa Salomo, mfalme wa Wayuda, nao wote wa milango ya Yuda na ya Benyamini nao wale watu waliosalia huku kwamba:
24
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Msipande kwenda kupigana na ndugu zenu, wana wa Isiraeli! Rudini kila mtu nyumbani kwake! Kwani jambo hili limefanywa na mimi. Walipolisikia neno hili la Bwana, wakarudi kwenda zao, kama Bwana alivyosema.
25
Yeroboamu akaujenga Sikemu milimani kwa Efuraimu, akakaa humo; kisha akatoka humo, akajenga Penueli.
26
Yeroboamu akasema moyoni mwake: Sasa ufalme utarudi kuwa wa mlango wa Dawidi,
27
watu wa huku wakipanda kwenda kutambikia Nyumbani mwa Bwana mle Yerusalemu; ndipo, mioyo ya watu wa huku itakapowageukia mabwana zao naye Rehabeamu, mfalme wa Wayuda, kisha wataniua, wapate kurudi kwa Rehabeamu, mfalme wa Wayuda.
28
Mfalme alipokwisha kulifanya shauri hilo akatengeneza ndama mbili za dhahabu, akawaambia watu: Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; Waisiraeli, itazameni miungu yenu iliyowatoa katika nchi ya Misri!
29
Ndama moja akaiweka Beteli, moja akaiweka Dani.
30
Jambo hili likawakosesha watu, kwani watu wakaenda hata Dani kuitambikia hiyo moja.
31
Hata vilimani juu akatengeneza vijumba vya kutambikia, akaweka nao watu wo wote kuwa watambikaji wasiokuwa na wana wa Lawi.
32
Yeroboamu akafanya sikukuu katika mwezi wa 8 siku ya 15 ya huo mwezi kama sikukuu ya Wayuda, naye akatoa ng'ombe za tambiko hapo pa kutambikia. Ndivyo, alivyofanya hata Beteli, azitambikie zile ndama, alizotengeneza; kisha akaweka Beteli watambikaji wa kutambika katika vijumba, alivyovijenga vilimani.
33
Napo hapo, alipopatengeneza pa kutambikia huko Beteli, akatoa ng'ombe za tambiko, ikawa ile siku ya 15 ya mwezi wa 8, aliyoizusha moyoni mwake; hapo, alipowafanyia wana wa Isiraeli sikukuu, akapanda kufika hapo pa kutambikia, avukize.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22