bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Kings 14
1 Kings 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 15 →
1
Siku zile Abia, mwana wa Yeroboamu, akaugua.
2
Ndipo, Yeroboamu alipomwambia mkewe: Inuka, Ujigeuzegeuze, watu wasikujue, ya kuwa ndiwe mkewe Yeroboamu; kisha nenda Silo! Tazama, huko yuko mfumbuaji Ahia aliyeniambia, ya kama nitakuwa mfalme wao walio ukoo huu.
3
Mkononi mwako uchukue mikate kumi na maandazi na kibuyu chenye asali, uende kwake! Yeye atakuambia yatakayokuwa ya huyu mtoto.
4
Mkewe Yeroboamu akafanya hivyo, kisha akaondoka, akaenda Silo, akaingia nyumbani mwa Ahia; lakini Ahia hakuweza kuona, kwani macho yake yalikuwa yametenda kiwi kwa ajili ya uzee wake.
5
Lakini Bwana alikuwa amemwambia: Tazama, mkewe Yeroboamu anakuja kukuuliza kwa ajili ya mwanawe, kwani yeye ni mgonjwa; nawe umwambie haya na haya! Naye atakapoingia atakuwa amejigeuzageuza kuwa kama mgeni.
6
Ikawa, Ahia aliposikia mashindo ya miguu yake, akiingia mlangoni, akamwambia: Karibu, mke wa Yeroboamu! Mbona unajigeuzageuza kuwa kama mgeni? Nami nimetumwa kukuambia neno gumu.
7
Nenda, umwambie Yeroboamu: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Nimekutoa katikati ya watu, nikakukweza, nikakupa kuwatawala walio ukoo wangu wa Waisiraeli,
8
nikaunyang'anya mlango wa Dawidi ufalme, nikakupa wewe; lakini hukuwa kama mtumishi wangu Dawidi aliyeyaangalia maagizo yangu, akaendelea kunifuata kwa moyo wake wote mzima, ayafanye hayo tu yanyokayo machoni pangu.
9
Lakini umefanya mabaya kuliko wote waliokuwa mbele yako, kwani umejiendea, ukajitengenezea miungu mingine na vinyago, unikasirishe, ukanitupa nyuma yako.
10
Lakini mtaniona, nikiuletea mlango wa Yeroboamu mabaya, niwatoweshe wa kiume walio wa Yeroboamu, kama watakuwa wamefungwa au kama watakuwa wamefunguliwa kwao Waisiraeli, nitawazoa walio wa mlango wa Yeroboamu, kama watu wanavyozoa mavi, hata wamalizike kabisa.
11
Wao wa Yeroboamu watakaokufa mjini mbwa watawala; nao watakaokufa shambani madege wa angani watawala, kwani Bwana amevisema.
12
Nawe inuka, uende nyumbani kwako! Hapo, miguu yako itakapoingia mjini, papo hapo mtoto atakufa.
13
Waisiraeli wote watamwombolezea, kisha watamzika, kwani kwao wa Yeroboamu huyu peke yake ndiye atakayeingia kaburini, kwani katika mlango wa Yeroboamu ni kwake tu kulikoonekana yaliyokuwa mema machoni pa Bwana.
14
Yeye Bwana atajiinulia mfalme wa Waisiraeli atakayeutowesha huu mlango wa Yeroboamu siku hiyo, nayo ya sasa siyo yayo hayo?
15
Ndipo, Bwana atakapowapiga Waisiraeli, kama matete yanavyotikiswa majini; atawang'oa Waisiraeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, awatawanye ng'ambo ya lile jito kubwa, kwa kuwa wamejitengenezea miti ya Ashera inayomkasirisha Bwana.
16
Atawatoa Waisiraeli kwa ajili ya makosa, Yeroboamu aliyoyakosa na kuwakosesha Waisiraeli nao.
17
Kisha mkewe Yeroboamu akaondoka, akaenda zake kufika Tirsa; alipoingia penye kizingiti cha nyumba, ndipo, yule kijana alipokufa.
18
Wakamzika, nao Waisiraeli wote wakamwombolezea, kama Bwana alivyosema kinywani mwa mtumishi wake mfumbuaji Ahia.
19
Mambo mengine ya Yeroboamu, jinsi alivyopiga vita, tena alivyotawala, tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli.
20
Siku, Yeroboamu alizokuwa mfalme, ni miaka 22; kisha akaja kulala na baba zake, naye mwanawe Nadabu akawa mfalme mahali pake.
21
Rehabeamu, mwana wa Salomo, akapata kuwa mfalme wa Wayuda; yeye Rehabeamu alikuwa mwenye miaka 41 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 17 mle Yerusalemu katika ule mji, Bwana aliouchagua katika mashina yote ya Isiraeli, alikalishe Jina lake humo. Jina la mama yake ni Nama aliyekuwa Mwamoni.
22
Wayuda wakayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, wakamchokoza kwa makosa yao, waliyoyakosa, maana yalikuwa mabaya kuliko yote, baba zao waliyoyafanya.
23
Nao wakajijengea vijumba vya kutambikia vilimani, wakajitengenezea nguzo za kutambikia na miti ya Ashera juu ya kila kilima kirefu na chini ya kila mti wenye majani mengi.
24
Hata wagoni wa patakatifu pao walikuwako katika nchi, wakayafanya matapisho yote ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele yao Waisiraeli.
25
Katika mwaka wa tano wa mfalme Rehabeamu ndipo, Sisaki, mfalme wa Misri, alipopanda kuujia Yerusalemu.
26
Akavichukua vilimbiko vya Nyumbani mwa Bwana navyo vilimbiko vya nyumbani mwa mfalme, vyote pia akavichukua, nazo ngao za dhahabu, Salomo alizozitengeneza, akazichukua.
27
Mahali pao mfalme Rehabeamu akatengeneza ngao za shaba, akazitia mikononi mwa wakuu wa wapiga mbio waliongoja pa kuingia nyumbani mwa mfalme, waziangalie.
28
Kila mara, mfalme alipoingia Nyumbani mwa Bwana, wapiga mbio wakazichukua, kisha wakazirudisha chumbani mwao wapiga mbio.
29
Mambo mengine ya Rehabeamu nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
30
Navyo vita vya kupigana kwao Rehabeamu na Yeroboamu vilikuwako siku zote.
31
Rehabeamu akaja kulala na baba zake, akazikwa kwa baba zake mjini mwa Dawidi, nalo jina la mama yake ni Nama aliyekuwa Mwamoni. Naye mwanawe Abiamu akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22