bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Kings 4
1 Kings 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 5 →
1
Mfalme Salomo akawa mfalme wa Waisiraeli wote;
2
nao hawa walikuwa wakuu wake: Azaria, mwana wa Sadoki, alikuwa mtambikaji.
3
Elihorefu na Ahia, wana wa Sisa, walikuwa waandishi; Yosafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa.
4
Benaya, mwana wa Yoyada, alikuwa mkuu wa vikosi, Sadoki na Abiatari walikuwa watambikaji.
5
Azaria, mwana wa Natani, alikuwa mkuu wa waangaliaji, naye mtambikaji Zabudi, mwana wa Natani, alikuwa mpenzi wa mfalme.
6
Ahisari alikuwa mkuu wa nyumbani, naye Adoniramu, mwana wa Abuda, alikuwa mkuu wa kazi za nguvu.
7
Salomo alikuwa na waangaliaji kumi na wawili waliowekwa kuwaangalia Waisiraeli wote, ndio waliompatia mfalme nao wa nyumbani mwake vyakula, ikawa kila mmoja akaleta vyakula vya mwezi mmoja katika mwaka.
8
Nayo majina yao ni haya: Mwana wa Huri milimani kwa Efuraimu;
9
mwana wa Dekeri alikuwako Makasi na Salabimu na Beti-Semesi na Eloni na Beti-Hanani.
10
Mwana wa Hesedi huko Aruboti, hata Soko na nchi yote ya Heferi ilikuwa yake.
11
Mwana wa Abinadabu vilima vyote vya Dori vilikuwa vyake, naye Tafati binti Salomo alikuwa mkewe.
12
Baana, mwana wa Ahiludi, yake ilikuwa Taanaki na Megido na Beti-Seani yote iliyoko kandokando ya Sartani chini ya Izireeli toka Beti-Seani hata Abeli-Mehola mpaka ng'ambo ya pili ya Yokimamu.
13
Mwana wa Geberi alikuwako vilimani kwa Gileadi; navyo vijiji vya Yairi, mwana wa Manase, vilivyoko Gileadi vilikuwa vyake, hata nchi ya Argobu iliyoko Basani, ni miji mikubwa 60 yenye maboma na makomeo ya shaba.
14
Ahinadabu, mwana wa Ido, alielekea Mahanaimu.
15
Ahimasi alikuwako Nafutali, naye alimchukua Basimati, binti Salomo, awe mkewe.
16
Baana, mwana wa Husai, alikuwako Aseri na Baloti.
17
Yosafati, mwana wa Parua, alikuwako Isakari.
18
Simei, mwana wa Ela, alikuwako Benyamini.
19
Geberi, mwana wa Uri, alikuwako katika nchi ya Gileadi iliyokuwa nchi ya Sihoni, mfalme wa Waamori, na ya Ogi, mfalme wa Basani. Naye mwangaliaji aliyewekwa katika nchi hizi alikuwa yeye mmoja.
20
Nao Wayuda na Waisiraeli walikuwa wengi, kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari ulivyo mwingi; walikuwa wakila, wakinywa na kufurahi.
21
Salomo akawa akizitawala nchi za kifalme zote kutoka lile jito kubwa kuifikia nchi ya Wafilisti hata mipaka ya Misri; walimletea mahongo, wakamtumikia Salomo siku zake zote za kuwapo.
22
Vyakula, Salomo alivyovitumia kwa siku moja, vilikuwa kori 30, ndio frasila 300 za unga mzuri na kori 60, ndio frasila 600 za unga mwingine;
23
tena ng'ombe 10 waliononeshwa na ng'ombe 20 wa malishoni na kondoo 100, tena kulungu na paa na funo na mabata waliononeshwa hawakuhesabiwa.
24
Kwani alikuwa akizitawala nchi zote za ng'ambo ya huku ya lile jito kutoka Tifusa hata Gaza, nao wafalme wote wa ng'ambo ya huku ya lile jito aliwatawala, kukawa na utengemano katika nchi zake zote zilizomzunguka.
25
Wayuda na Waisiraeli wakakaa na kutulia kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mkuyu wake kutoka Dani kufikia Beri-Seba siku zote, Salomo alizokuwapo.
26
Salomo alikuwa na majozi ya farasi 40000 ya magari yake, tena wapanda farasi 12000.
27
Nao wale waangaliaji wakampatia mfalme Salomo vyakula nao wote walioikaribia meza ya mfalme Salomo, kila mmoja wao mwezi wake, hawakuwakosesha kitu cho chote.
28
Nao mtama na mabua ya ngano ya farasi wa kupanda na wa magari wakayapeleka mahali hapo, alipokuwa, kila mtu hapo, alipoagizwa.
29
Mungu akampa Salomo werevu wa kweli na utambuzi mwingi sana na akili za moyo zilizokuwa nyingi kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari.
30
Werevu wa kweli wa Salomo ukazidi kuliko werevu wao wote waliokuwa werevuwa kweli upande wa maawioni kwa jua, nao warevu wote wa kweli ulioko Misri.
31
Akawa mwerevu wa kweli kuliko watu wote pia, akamshinda naye Etani wa Ezera na Hemani, hata Kalkoli na Darda, wana wa Maholi; jina lake likasifiwa katika mataifa yote pande zote.
32
Akasema mifano 3000, nazo nyimbo zake zikawa 1005.
33
Akaiimbia miti kuanzia miangati iliyoko Libanoni kufikisha hata mivumbasi imeayo mahameni, akawaimbia nao nyama wa porini na ndege na wadudu na samaki.
34
Watu wakaja na kutoka katika makabila yote, wausikilize werevu wa kweli wa Salomo, wakatoka hata kwa wafalme wote wa huku nchini waliopata habari ya werevu wake wa kweli.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22