bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Kings 17
1 Kings 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 18 →
1
Elia wa Tisibe aliyekaa ugenini huko Gileadi akamwambia Ahabu: Hivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli, ninayemtumikia, alivyo Mwenye uzima, miaka hii umande hautakuwako, wala mvua haitakunya, isipokuwa kwa neno la kinywa changu.
2
Kisha neno la Bwana likamjia la kwamba:
3
Ondoka hapa, ujiendee upande wa maawioni kwa jua kijificha kwenye kijito cha Kriti kinachoingia Yordani!
4
Na unywe katika kijito hicho, tena nimeagiza makunguru, wakutunze kuko huko.
5
Ndipo, alipokwenda, afanye, kama Bwana alivyomwagiza, akaenda kukaa kwenye kijito cha Kriti kinachoingia Yordani.
6
Makunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, tena mkate na nyama jioni, akanywa maji ya hicho kijito.
7
Ikawa, siku zilipopita, kijito kikakauka, kwani hakuna mvua katika nchi.
8
*Ndipo, neno la Bwana lilipomjia la kwamba:
9
Inuka, uende Sareputa katika nchi ya Sidoni, ukae huko! Utaona huko mwanamke mjane, niliyemwagiza, akutunze.
10
Akainuka, akaenda Sareputa. Alipofika penya lango la mji akaona huko mwanamke mjane aliyeokota kuni, akamwita na kumwambia: Uniletee maji kidogo katika kata, ninywe!
11
Alipokwenda kuyaleta, akamwita na kumwambia: Uniletee hata kipande kidogo cha mkate mkononi mwako.
12
Akamjibu: Hivyo, Bwana Mungu wako alivyo Mwenye uzima, sinacho kilichochomwa! Nilivyo navyo ndio gao la unga katika kitungi na vifuta vichache katika kichupa. Tazama, ninaokota vikuni viwili, nije nijipikie mwenyewe na mwanangu, tule, kisha tufe.
13
Elia akamwambia: Usiogope! Nenda, ufanye, kama ulivyosema! Lakini kwanza unitengenezee kiandazi kidogo, uniletee hapa nje! Kisha ujitengenezee wewe na mwanao!
14
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Unga hautaisha katika kitungi, wala kichupa hakitakosa mafuta mpaka siku ile, Bwana atakaponyesha mvua katika nchi.
15
Yule mwanamke akenda, akafanya, kama Elia alivyosema, akala yeye, naye Elia aliyekuwamo nyumbani mwake siku kwa siku.
16
Lakini unga haukuisha katika kitungi, wala kichupa hakikukosa mafuta, kama Bwana alivyosema kinywani mwa Elia.*
17
Ikawa, hayo yalipokwisha kufanyika, mwanawe huyu mwanamke aliyekuwa mwenye nyumba akaugua, nao ugonjwa wake ukawa wenye nguvu sana, hata pumzi hasikusalia mwilini mwake.
18
Ndipo, mwanamke alipomwambia Elia: Tuko na bia gani mimi na wewe, mtu wa Mungu? Umeingia mwangu kuyaumbua mabaya yangu, niliyoyafanya, umwue mwanangu.
19
Elia akamwambia: Nipe mwanao! Akamchukua kifuani pake, akapanda naye darini, alimokuwa anakaa, akamlaza kitandani pake.
20
Akamlilia Bwana kwamba: Bwana Mungu wangu, mbona umemfanyizia vibaya naye huyu mwanamke, ambaye nimefikia kwake, ukimwua mwanawe?
21
Akamkumbatia mtoto mara tatu na kumlalia juu, akamlilia Bwana akisema: Bwana Mungu wangu, roho ya huyu mtoto na irudi mwake!
22
Bwana akaiitikia sauti ya Elia, roho ya mtoto ikarudi mwilini mwake, akawa mzima tena.
23
Ndipo, Elia alipomchukua mtoto, akashuka naye nyumbani kutoka darini, akampa mama yake yeye Elia akimwambia: Tazama, mwanao ni mzima!
24
Yule mwanamke akamwambia Elia: Sasa hivi nimetambua, ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, nalo Neno la Mungu lililomo kinywani mwako ni la kweli.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22