bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Kings 5
1 Kings 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 6 →
1
Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma watumishi wake kwa Salomo, kwani alisikia, ya kuwa wamempaka mafuta, awe mfalme mahali pa baba yake, kwani Hiramu alikuwa akimpenda Dawidi siku zote.
2
Salomo akatuma kwa Hiramu kumwambia:
3
Wewe unajua, ya kuwa baba yangu Dawidi hakuweza kulijengea Jina la Bwana Mungu wake nyumba kwa ajili ya vita, adui zake walivyomletea toka pande zote, hata Bwana akawaweka chini ya nyayo za miguu yake.
4
Sasa Bwana Mungu wangu amenipa kutulia pande zote, hakuna mpingani wala jambo baya.
5
Kwa hiyo nimesema, nilijengee Jina la Bwana Mungu wangu nyumba, kama Bwana alivyomwambia baba yangu Dawidi kwamba: Mwanao, nitakayempa kukaa mahali pako katika kiti chako cha kifalme, ndiye atakayelijengea Jina langu nyumba.
6
Sasa agiza, watu wanikatie miangati huko Libanoni! Watu wangu na wachanganyike na watu wako, nao mshahara wote wa watu wako nitakupa, kama utakavyosema, kwani mwenyewe unajua, ya kuwa kwetu hakuna ajuaye kuchonga miti kama watu wa Sidoni.
7
Ikawa, Hiramu alipoyasikia haya maneno ya Salomo akafurahi sana, akasema: Bwana na atukuzwe leo hivi, kwani amempa Dawidi mwana mwenye werevu wa kweli wa kuwatawala wale watu wengi.
8
Ndipo, Hiramu alipotuma kwa Salomo kumwambia: Nimeyasikia maneno yako, uliyotuma kuniambia. Mimi nitayafanya yote, uyatakayo, nikupatie miti ya miangati na miti ya mivinje.
9
Watu wangu wataitelemsha toka Libanoni hata baharini; kisha mle baharini nitaifunga, ielee; ndivyo, nitakavyoifikisha mahali pale, utakaponiambia; hapo nitaifungua tena, wewe upate kuichukua. Nawe na uyafanye, niyatakayo, ukiwapa watu wa kwangu vyakula.
10
Kisha Hiramu akampa Salomo miti ya miangati na miti ya mivinje, yote kama alivyoitaka.
11
Naye Salomo akampa Hiramu kori 20000, ndio frasila 200000 za ngano kuwa posho za watu wa kwake na kori 20, ndio frasila 200 za mafuta mazuri mno; hivi ndivyo, Salomo alivyompa Hiramu mwaka kwa mwaka.
12
Bwana akampa Salomo werevu wa kweli, kama alivyomwambia. Kwao Hiramu na Salomo yakawako matengemano, wakafanya agano hao wawili.
13
Kisha mfalme Salomo akawatoza Waisiraeli wote watu wa kazi za nguvu, nao hao watu wa kazi za nguvu wakawa watu 30000.
14
Akatuma kila mwezi watu 10000 kwenda Libanoni, wapokeane hivyo: mwezi mmoja wakae Libanoni, kisha nyumbani kwao miezi miwili. Naye Adoniramu alikuwa mkuu wao hao watu wa kazi za nguvu.
15
Salomo akawa nao wachukuzi wa mizigo 70000, tena wachonga mawe 80000 milimani.
16
Tena Salomo akawa na wasimamizi 3300 waliowekwa naye kuwa wakuu wa wafanya kazi na kuwasimamia, wakifanya kazi.
17
Mfalme akaagiza, wavunje mawe yaliyo makubwa na mazuri mno ya kuchonga ya kuwekea misingi ya nyumba.
18
Waashi wa Salomo na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga. Ndivyo, walivyotengeneza miti na mawe, wapate kuijenga hiyo nyumba.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22