bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ephesians 1
Ephesians 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 2 →
1
Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, nawaandikia ninyi watakatifu mlioko Efeso, nanyi mliomtegemea Kristo Yesu:
2
Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo!
3
*Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetugawia mema yote ya kiroho yatokayo mbinguni kwake Kristo!
4
Kwani ulimwengu ulipokuwa haujaumbwa bado, alituchagua sisi kuwa wake yeye, tuwe watakatifu machoni pake pasipo kilema.
5
Kwa hivyo, anavyotupenda, alitutenga kale, tupokelewe kuwa wana wake mwenyewe tukimfuata Yesu Kristo; ndiyo yaliyompendeza, akayataka, yawepo.
6
Nasi huusifu utukufu wa kipaji chake, alichotugawia hapo, alipomtoa mpendwa wake.
7
Katika damu yake yeye ndimo, tupatiamo ukombozi, maana twaondolewa makosa; hayo ndiyo magawio yake mengi
8
yaliyotuongezea nasi werevu wote ulio wa kweli, hata ujuzi wote.
9
Kisha akatutambulisha, ayatakayo, yaliyokuwa yamefichwa. Ndivyo, ylivyompendeza, akayaweka kale moyoni mwake,
10
yatengenezeke, siku alizoziweka zitakapotimia, Kristo awe kichwa chao yote yaliyoko mbinguni nacho chao yaliyoko nchini.
11
Yeye ndiye, ambaye tulipatiwa naye urithi wetu, tuliokatiwa kale na kuwekewa kale, maana yeye huyafanya yote, yawepo, kama ayatakavyo mwenyewe.
12
Kwa hiyo sisi tuliotangulia kumngojea Kristo ndio tutakaousifu utukufu wake.
13
Nanyi mmelisikia Neno la kweli, ni ule Utume mwema wa wokovu wenu; napo hapo, mlipolitegemea, mlitiwa muhuri yake mlipompata Roho Mtakatifu, tuliyeagiwa.
14
Huyu ni rehani ya urithi wetu, tujue: tumekombolewa, tu watu wake, utukufu wake upate wenye kuusifu.*
15
*Kwa hiyo mimi niliposikia, mnavyomtegemea Bwana Yesu, tena mnavyowapenda watakatifu wote,
16
sichoki kushukuru kwa ajili yenu kila, niwakumbukapo nikiomba.
17
Nawaombea, Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye utukufu, awape roho ya werevu wa kweli na ya ufunuzi, mmtambue yeye alivyo.
18
Namo mioyoni mwenu atiemo macho yaliyoangazwa, mpate kujua, kilivyo hicho kingojeo, mlichoitiwa naye, tena mwujue nao utukufu wa urithi wake, aliowawekea watakatifu, ulivyo mwingi.
19
Mpate kuujua nao uwezo wake, unavyokua kuupita wote mwingine ulioko; huo akatupa sisi tumtegemeao kwa kuhimizwa na nguvu zake kuu.
20
Ndizo, alizozitumia alipomfufua Kristo katika wafu na kumketisha kuumeni kwake mbinguni
21
na kumpa cheo kuupita ukubwa na ufalme na uwezo na ubwana wote na kuyapita majina yo yote yatakayotajwa siku hizi, nazo siku zote zitakazokuja.
22
Akayaweka yote kuwa chini migguni pake, naye mwenyewe akamfanya kuwa mkuu peke yake, awe kichwa chao wateule wote,
23
maana wao ni mwili wake; huu ndio utimilifu wake yeye anayeyatimiza yote pia kwao wote po pote pasipo kusaza.*
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6