bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ephesians 5
Ephesians 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 6 →
1
Mwigeni Mungu, kama inavyowapasa watoto wapendwa!
2
Tena mwendeane na kupendana, kama Kristo alivyowapenda ninyi! Akajitoa kwa ajili yetu sisi kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuuawa, Mungu asikie mnuko mzuri.
3
Lakini mambo ya ugoni na ya uchafu wo wote na ya choyo yasitajwe kwenu kamwe, kama inavyowapasa watakatifu;
4
wala matusi wala mapuzi wala mafyozi mabaya, maana siyo yafaayo; yafaayo ni ya kushukuru.
5
Kwani haya yajueni na kuyatambua vema: hakuna mgoni wala mchafu wala mwenye choyo aliye mtambikia vinyago atakayepata fungu katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.
6
Pasioneke mwenye kuwadanganya na maneno yasiyo na maana! Kwani kwa ajili yao makali ya Mungu huwajia wakataao kutii.
7
Kwa hiyo msichanganyike nao!
8
Kwani kale mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa mwanga kwa kuwa naye Bwana. Mwendelee, kama iwapasavyo wana wa mwanga!
9
Kwani matunda yanayozaliwa mwangani ndio wema wo wote na wongofu na ukweli.*
10
Pambanueni, kama ni mambo gani yampendezayo Bwana!
11
Msiwe wenzao wenye kuzifanya kazi za giza zisizofaa, ila mkaze kuwaumbua!
12
Kwani hutia soni kuyataja tu yanayofanywa nao na kuyafichaficha.
13
Lakini yote hufunuliwa yakiumbuliwa na mwanga, kwani kila kitu kinachofunuliwa huangazika.
14
Kwa hiyo husema: Amka, wewe uliyelala! Inuka, utoke kwenye wafu! Kisha Kristo atakuangaza.
15
*Kwa hiyo angalieni sana, mtakavyoendelea! Msiwe wenye ujinga, ila mwe wenye werevu wa kweli!
16
Mzitumie vema siku za sasa! Kwani siku hizi ndizo mbaya.
17
Kwa hiyo msipumbae, ila mjijulishe, Bwana ayatakayo!
18
Wala msilewe pombe! Kwani hazikomeki tena! Ila mjijaze Roho!
19
Mwongeleane na kuambiana shangwe na nyimbo na tenzi za Kiroho, mkimwimbia Bwana na kumshangilia mioyoni mwenu,
20
mkamshukuru Mungu Baba po pote kwa ajili yao yote, mliyoyapata katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo!
21
Kisha na mnyenyekeane kila mtu na mwenziwe kwa hivyo, mnavyomwogopa Kristo!*
22
Ninyi wanawake, watiini waume wenu, kama mnavyomtii Bwana!
23
Kwani mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo alivyo kichwa chao wateule, maana yeye ndiye aliyeuokoa mwili.
24
Lakini kama wateule wanavyomtii Kristo, vivyo hivyo nao wake sharti wawatii waume wao katika mambo yote!
25
Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyowapenda wateule, akajitoa mwenyewe kwa ajili yao,
26
awatakase na kuwang'aza akiwaosha maji, kama alivyoagana nao.
27
Ndivyo, alivyotaka kujitengenezea mwenyewe wateule wenye tukuzo hilo la kwamba: Hawanalo doa wala kunjo wala lo lote lifananalo nayo yaliyo hivyo, maana ndio watakatifu pasipo kilema.
28
Ndivyo, inavyowapasa nao waume kuwapenda wake zao, kama ni miili yao. Kwani mwenye kumpenda mkewe hujipenda mwenyewe.
29
Kwani toka kale hakuna mtu ye yote aliyeuchukia mwili wake mwenyewe, ila huulea na kuutunza, kama Kristo naye anavyowafanyia wateule;
30
kwani sisi tu viungo vya mwili wake.
31
Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake, agandamiane na mkewe, nao hao wawili watakuwa mwili mmoja.
32
Fumbo hili ni gumu la kulifumbua, lakini mimi nasema la Kristo na la wateule!
33
Lakini hata ninyi kila mmoja wenu na ampende mkewe, kama anavyojipenda mwenyewe! Lakini mke amche mumewe!
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6