bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ephesians 6
Ephesians 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
1
*Ninyi watoto, watiini wazazi wenu, kwa kuwa mnaye Bwana! Kwani hivi huongoka:
2
Mheshimu baba yako na mama yako! Nalo ni agizo la kwanza lenye kiagio cha kwamba:
3
Upate kukaa vema, nazo siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi!
4
Nanyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu! Ila mwakuze na kuwaonya, wamche Bwana!
5
Ninyi watumwa, kama mnavyomtii Kristo, watiini nao mabwana zenu wa nchini kwa kuwaogopa na kutetemeka, mkilishika mioyoni mwenu lile Neno moja tu!
6
Msifanye kazi nzuri machoni pao tu kama watakao kuwapendeza watu, ila kama watumwa wake Kristo myafanye kwa mioyo, Mungu ayatakayo!
7
Tumikeni na kuuitikia utumishi, kama sio watu, mnaowatumikia, ila kama ni Bwana, mmtumikiaye!
8
Tena mjue: kila mtu akifanya kazi njema yo yote atalipwa naye Bwana, akiwa mtumwa, au akiwa mwungwana.
9
Nanyi mabwana, mwafanyie yaleyale! Mwache kuwatisha mkijua: mbinguni yuko aliye Bwana wao na wenu, tena kwake hakuna upendeleo!*
10
*Mwisho, ndugu zangu, kwa sababu m wake Kristo, mwe wenye kushupaa kwa nguvu ya uwezo wake!
11
Yashikeni mata yote ya Kimungu, mweze kusimama na kuyakinga madanganyo yake msengenyaji!
12
Kwani vita vyetu, tuvipiganavyo, sivyo vya wenye damu na miili, ila ni vya kupigana nao wafalme na wenye uwezo na wenye kutawala nchini penye giza, nao wale pepo wabaya waliopo angani.
13
Kwa hiyo yashikeni mata ya Kimungu yote, mweze kusimama penye mapigano, siku mbaya itakapokuwapo, mpate kuyashinda mabaya yote mkiwa mmesimama vivyo hivyo!
14
Simameni mkiwa mmejifunga ukweli viunoni! Vifuani vaeni wongofu, uwe kanzu yenu ya chuma!
15
Miguuni vaeni viatu! Hivyo mtakuwa tayari kuutangaza utume mwema wa utengemano.
16
Kuliko hayo yote kazeni kumtegemea Mungu, kuwe ngao yenu ya kuizima mishale yote yenye moto ya yule Mbaya!
17
Kichwani vaeni wokovu, uwe kofia yenu ngumu! Kisha shikeni nao upanga wa Kiroho, ndio neno la Mungu!*
18
Tena kwa ajili ya mambo yote mwombe na kubembeleza siku zote kwa nguvu ya Roho! Tena kesheni, myaweze hayo, mkijipingia kuwaombea watakatifu wote!
19
Niombeeni nami, nipate kufumbuliwa kinywa changu, niseme na kulitambulisha waziwazi fumbo la Utume mwema, ambao ninautumikia
20
namo humu kifungoni, nipate kuutangaza pasipo woga, kama inavyonipasa!
21
Lakini kusudi mpate kujua nanyi, mambo yangu yalivyo, nami mwenyewe nilivyo, yote atawasimulia Tikiko aliye ndugu yetu mpendwa na mtumishi mwelekevu wa Bwana.
22
Huyu nimemtuma, aje kwenu kwa ajili hiihii, myatambue, mambo yetu yalivyo, naye aitulize mioyo yenu.
23
Ndugu, mtengemane na kupendana, mpate hata nguvu ya kumtegemea Mungu itokayo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo!
24
Upole uwakalie wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo pasipo kulegea! Amin.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
All chapters:
1
2
3
4
5
6