bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Galatians 1
Galatians 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 2 →
1
Mimi Paulo ni mtume, lakini sikutumwa na watu wala kwa agizo la mtu, ila nimetumwa kwa agizo lake Yesu Kristo nalo lake Mungu Baba aliyemfufua katika wafu.
2
Mimi pamoja na ndugu wote walio pamoja nami tunawaandikia ninyi wateule wa Galatia.
3
Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo!
4
Ndiye aliyejitoa kwa ajili ya makosa yetu, apate kutuokoa katika dunia hii mbaya ya sasa. Ndivyo, Mungu, Baba yetu, alivyotaka.
5
Huyu atukuzwe kale na kale pasipo mwisho! Amin.
6
Nastaajabu, ya kuwa mwageuzwa upesi hivyo, mwondoke kwake yeye aliyewaita, mgawiwe kipaji chake Kristo, mkafuata utume mwema mwingine.
7
Tena hakuna utume mwema mwingine, ila wako watu tu wanaowahangaisha; ndio wanaotaka kuugeuza Utume mwema wa Kristo.
8
Lakini ikiwa sisi, au ijapo malaika wa mbinguni, akiwatangazia utume mwema mwingine kuliko ule, tuliowapigia sisi, na awe ameapizwa!
9
Tuliyoyasema sasa hivi, narudia kuyasema tena: Mtu akiwatangazia utume mwema mwingine kuliko ule, mlioupokea, na awe ameapizwa!
10
Je? Hayo nayasemea kuitikiwa nao watu au naye Mungu? Au je? Natafuta kuwapendeza watu? Kama ningependeza watu bado, basi, singekuwa mtumwa wake Kristo.
11
Ndugu zangu, nawatambulisha, ya kuwa Utume mwema uliotangazwa nami sio wa kimtu.
12
Kwani nami sikuupokea kwa mtu, wala sikufundishwa, ila nimefunuliwa na Yesu Kristo.
13
Kwani mmesikia, nilivyoendelea hapo, nilipolifuata tambiko la Kiyuda, ya kuwa nalijipingia kuwafukuza wateule wa Mungu na kuwajengua.
14
Nami hapo, nilipolifuata tambiko la Kiyuda, nikapita wenzangu wengi, ambao tulizaliwa nao mwaka mmoja, maana nilikaza kujihimiza, niandamane nayo, tuliyoyapokea kwa baba zetu.
15
Lakini Mungu alikuwa amenitenga hapo, nilipokuwa tumboni mwa mama yangu, akaniita, nigawiwe kipaji chake.
16
Hapo, alipopendezwa kumfunua Mwana wake moyoni mwangu, kusudi nije, niwapigie wamizimu hiyo mbiu yake njema, papo hapo nikakata mawazo pasipo kuuliza mwili wangu ulio wenye nyama na damu,
17
wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwao waliokuwa mitume mbele yangu, ila nalikwenda Arabuni, kisha nikarudi tena Damasko.
18
Miaka mitatu ilipokwisha kupita, nikapanda kwenda Yerusalemu, nijuane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano.
19
Lakini hakuna mtume mwingine, niliyemwona, asipokuwa Yakobo, nduguye Bwana.
20
Lakini haya, ninayowaandikia, tazameni, Mungu anayajua, ya kuwa sisemi uwongo.
21
Kisha nikafika upande wa Ushami na Kilikia.
22
Nami nilikuwa sijajulikana uso kwa uso nao wateule wake Kristo walioko Yudea.
23
Ila walikuwa wamesikia tu: Yule aliyetufukuza kwanza sasa huipiga hiyo mbiu njema ya kumtegemea Bwana, alikokuwa amekujengua. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6