bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Galatians 6
Galatians 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
1
Ndugu, mtu akipatikana ameanguka, ninyi mlio wa Kiroho, mwonyeni Kiroho kwa upole, ashupae tena! Jiangalie mwenyewe, usijaribiwe nawe!
2
Mchukuliane mizigo! Hivyo mtayatimiza Maonyo yake Kristo.
3
Kwani mtu akijiwazia kuwa mwenye nguvu, tena siye, hujidanganya mwenyewe.
4
Lakini kila mtu azitazame kazi zake mwenyewe, ziwe nzuri! Ndipo, atakapojivuma moyoni tu, asitolee wengine majivuno yake.
5
Kwani kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
6
Lakini mwenye kufundishwa lile Neno na amgawie mfunzi mema yote, aliyo nayo!
7
Msidanganyike, Mungu habezwi! Kwani mtu aliyoyapanda, ndiyo, atakayoyavuna.
8
Maana mwenye kupanda mwilini mwake atavuna humo mwilini kuoza. Lakini mwenye kupanda Rohoni atavuna humo Rohoni uzima wa kale na kale.
9
Tusichoke kuyafanya yaliyo mazuri, kwani siku zake zitakapotimia, tutavuna pasipo kukoma.
10
Basi, kwa sababu tuko nchini bado, wote na tuwatendee mema, lakini kuliko wengine wenzetu wa kumtegemea Bwana!*
11
Yatazameni haya maandiko yote, niliyowaandikia kwa mkono wangu mimi!
12
Wote wanaotaka kupendeleza miili, hao huwashurutisha kutahiriwa; tena hapana neno jingine, ni kwamba tu: Wasifukuzwe kwa ajili ya msalaba wake Kristo.
13
Kwani nao wenyewe waliotahiriwa hawayashiki Maonyo, ila hutaka, ninyi mtahiriwe, wapate kujivunia miili yenu.
14
Lakini mimi sitaki kujivuna, isipokuwa kwa ajili ya msalaba wake Bwana wetu Kristo, maana mlemle mimi nimefiwa na ulimwengu, nao ulimwengu umefiwa na mimi mlemle.
15
Kwani ukiwa naye Kristo Yesu, kutahiriwa siko, wala kutotahiriwa siko, ila kuwa kiumbe kipya ndiko.
16
Nao wote wanaoendelea na kujipingia hivyo na watengemane, upole uwakalie pamoja nao Waisiraeli wa Mungu!
17
Basi, tangu sasa asionekane atakayenisumbua tena! Kwani mwilini mwangu mimi ninayo makovu ya Yesu.
18
Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uzikalie roho zenu, ndugu! Amin.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
All chapters:
1
2
3
4
5
6