bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Galatians 4
Galatians 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 5 →
1
Nasema: Kibwana siku anapokuwa mchanga bado, hakuna, apitanacho na mtumwa, angawa ni bwana wa vyote,
2
ila hana budi kuwatii walezi na watunza mali, mpaka siku zitimie zilizowekwa na baba yake.
3
Vivyo hivyo nasi tulipokuwa wachanga tulikuwa tumeyatumikia kitumwa mambo ya kwanza ya humu ulimwenguni.
4
Lakini siku zilipotimia, Mungu alimtuma Mwanawe, akizaliwa na mwanamke, akawa akiyatii Maonyo,
5
kusudi awakomboe walioyatii Maonyo, kwamba tupate kuwa wana.
6
Kwa sababu m wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe, aingie mioyoni mwetu, ndiye anayetuombea na kulia: Ee, Baba yetu!
7
Kwa hiyo hu mtumwa tena, ila umekuwa mwana. Lakini kama umekuwa mwana, umekuwa hata mrithi wa Mungu kwa kuwa wake Kristo.*
8
Lakini hapo kale, mlipokuwa hammjui Mungu, mlitumikia miungu isiyo miungu kwa hivyo, ilivyo.
9
Lakini sasa, mnapomtambua Mungu, tena mnapotambulikana kwake Mungu, mwaigeukiaje tena ile miiko ya kale ikosayo nguvu, iletayo ukiwa tu? Mwatakaje, mwanze kuitumikia tena?
10
Mwaangalia sana siku na miezi na miongo na miaka.
11
Naogopa kwa ajili yenu kwamba: Labda nimejisumbua kwenu bure.
12
Ndugu, nawabembeleza, mwe, kama mimi nilivyo! Maana, mimi ni kama ninyi. Hamkunipotoa lo lote.
13
Lakini mwajua: hapo kwanza nilipowapitia hiyo mbiu njema nilikuwa mnyonge wa mwili;
14
nikawapo nikijaribiwa na mambo yale ya mwili wangu, lakini hamkunibeua, wala hamkunifukuza, ila mmenipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu mwenyewe.
15
Yale mashangilio yenu sasa yako wapi? Kwani nawashuhudia ninyi kwamba: Kama ingaliwezekana, mngaliyang'oa hata macho yenu, mkanipa.
16
Je? Nimegeuka kuwa mchukivu wenu kwa kuwaambia yaliyo ya kweli?
17
Wanavyowahimiza, si vizuri, ila wanataka kuwatenganisha na sisi, mpate kujihimiza kuwatumikia wao.
18
Ni vizuri kujihimiza kwa ajili ya jambo zuri po pote, msijihimize hapo tu, nikiwako kwenu.
19
Watoto wangu, ninao uchungu, kama nitawazaa mara ya pili, mpaka Kristo aonekane kuwa yumo mwenu.
20
Ingefaa, niwe kwenu sasa, nikaweza kuigeuza sauti yangu, maana ninawahangaikia ninyi.
21
Mniambie ninyi mnaotaka kujitwika Maonyo: Hamyasikii Maonyo?
22
Kwani imeandikwa: Aburahamu alikuwa na wana wawili waume, mmoja wa kijakazi, mmoja wa mkewe mwenyewe.
23
Lakini yule wa Kijakazi alizaliwa kwa tamaa ya mwili, lakini yule wa mwungwana alizaliwa kwa nguvu ya kiagio
24
Mambo hayo yako na maana: kwani wale wanawake wawili ndio maagano mawili. La kwanza ndilo lililotokea mlimani kwa Sinai, linalozaa watumwa tu; hili ndio Hagari.
25
Maana mlima wa Sinai huitwa Hagari kule Arabuni; nao umelingana na Yerusalemu wa sasa, kwani uko utumwani pamoja na watoto wake.
26
Lakini ule Yerusalemu wa juu ndio yule mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.
27
Kwani imeandikwa: Shangilia, wewe uliye mgumba, usiyezaa! Jichekelee na kupaza sauti, wewe usiyeona uchungu wa kuzaa! Kwani wana wake yule aliye peke yake ni wengi kuliko wana wake yule aliye na mumewe.
28
Lakini ninyi ndugu, mmekuwa wana wa kiagio kama Isaka.
29
Lakini kama hapo kale yule aliyezaliwa kwa tamaa ya mwili alivyomchokoza yule aliyezaliwa kwa nguvu ya Roho, ndivyo, vilivyo hata sasa.
30
Lakini Maandiko yasemaje? Mfukuze huyu kijakazi pamoja na mwanawe! Kwani mwana wa kijakazi hatapata urithi pamoja na mwana wa mwungwana.
31
Kwa hiyo, ndugu, sisi hatu watoto wa kijakazi, ila wake mwungwana.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6