bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Micah 1
Micah 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 2 →
1
Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Mika wa Moreseti siku zile, Yotamu na Ahazi na Hizikia walipokuwa wafalme wa Yuda, ni ono lake la mambo yatakayoijia miji ya Samaria na ya Yerusalemu.
2
Sikieni, ninyi makabila yote! Sikilizeni, nchi nao wote walioko! Bwana Mungu na atoe ushahidi wa kuwashinda ninyi akitokea katika Jumba lake takatifu.
3
Kwani mtamwona Bwana, akiondoka mahali pake, akishuka akikanyaga juu ya vilima vya nchi.
4
Ndipo, milima itakapoyeyuka chini yake, nayo mabonde yataatuka nyufa; itayeyuka kama nta motoni, iwe kama maji yaporomokayo magengeni.
5
Hayo yote yatakuja kwa ajili ya upotovu wa Yakobo, na kwa ajili ya makosa yao walio mlango wa Isiraeli. Upotovu wa Yakobo ndio nini? Sio ule wa Samaria? Napo pa kutambikia vilimani ndipo wapi? Sipo Yerusalemu?
6
Kwa hiyo nitaugeuza Samaria, uwe chungu la mawe shambani pa kupandia mizabibu, nayo mawe yake nitayaporomosha bondeni, niifunue misingi yake, iwe wazi.
7
Vinyago vyao vyote vya kuchonga vitakatwakatwa, nayo mishahara ya ugoni itateketezwa kwa moto; vinyago vyao vyote pia nitavitoa, viharibiwe, kwani wamevipata vyote kuwa mshahara wa ugoni, navyo vitakuwa mshahara wa ugoni tena.
8
Hayo ndiyo, ninayotaka kuyaombolezea na kupiga vilio nikitembea pasipo nguo kuwa mwenye uchi kabisa, nifanye maombolezo kama mbweha na kupiga vilio kama wana wa mbuni.
9
Kwani mapigo yako hayaponi, yatamfikia naye Yuda, yatagonga hata malangoni kwao, walio ukoo wangu, mle malangoni mwa Yerusalemu.
10
Msiyasimulie Gati (Penye Masimulio), msilie kabisa! Gaagaeni uvumbini Beti-Leafura (Nyumba ya Uvumbi)!
11
Jiendeeni mkaao Safiri (Mji wa Mapambo) na kuona soni kwa kuwa wenye uchi! Wakaao Sanani (Matokeo) hawatoki tena, maombolezo ya Beti-Haeseli (Nyumba ya Wanyimaji) yatawanyima fikio.
12
Wakaao Maroti (Uchungu) wanaona uchungu kwa ajili ya mema yao, kwani mabaya yameyashukia malango ya Yerusalemu toka kwa Bwana.
13
Gari la vita lifungie farasi wenye mbio, ukaaye Lakisi (Panapopigwa Mbio)! Kwani huko ndiko, binti Sioni alikoanzia kukosa, kwani kwao ndiko, mapotovu ya Isiraeli yalikoonekana.
14
Kwa hiyo huna budi kutoa vipaji vya kuachana, uwape wa Moreseti-Gati (Uchumba wa Gati). Nyumba za Akizibu (Madanganyo) zitawadanganya wafalme wa Isiraeli.
15
Ninyi mkaao Maresa (Wenyeji) nitawaletea mwenyeji wa kweli, utukufu wa Isiraeli utajiendea mpaka Adulamu.
16
Jikatie nywele, uwe mwenye kipara kwa ajili ya watoto wako waliokupendeza! Kikuze sana kipara chako, kiwe kama cha ngusu, kwani wametekwa na kuhamishwa kwako.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7