bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Micah 2
Micah 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 3 →
1
Yatawapata wanaowaza maovu, watungao mabaya vitandani mwao, wayafanye asubuhi kutakapopambazuka, mikono yao ikiweza kuyamaliza.
2
Kwa kutamani mashamba huyanyang'anya; ikiwa nyumba, huzichukua nazo, humkorofisha mwenye nyumba pamoja nao waliomo, vilevile mwenye shamba, ijapo liwe fungu lake.
3
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtayaona mabaya, ninayouwazia mlango huu! Yakiwapata, hamtaweza kuzitoa shingo zenu mle, wala hamtaweza kwenda na kuzinyosha shingo zenu, kwani siku hizo zitakuwa mbaya kweli.
4
Siku hiyo watawatungia ninyi mfano, wataomboleza ombolezo la kwamba: Imefanyika! Tumeangamizwa! Mafungu yao walio ukoo wangu anawapa wengine! Kumbe mimi ameninyang'anya mashamba yetu, awagawie wao wamkataao!
5
Kwa hiyo hamtapata tena katika mkutano wa Bwana atakayempimia mtu fungu, alilolipata kwa kura.
6
Wao huhubiri: Msihubiri! Haifai kuhubiri mambo kama hayo, matusi nayo hayakomi!
7
Je? Sio walio mlango wa Yakobo wanaosema: Inakuwaje? Roho yake Bwana ni nyepesi ya kukasirika? Au matendo yake ni yayo hayo? Hasemi: Ninamwendea kwa wema ashikaye njia inyokayo?
8
Lakini tangu kale mmewainukia walio ukoo wangu, kama ni adui zenu; wapitao pasipo mawazo mabaya mwawavua kanzu za juu na mavazi ya ndani, kama ni mateka ya vitani.
9
Wanawake wao walio ukoo wangu mwawafukuza katika nyumba zao zilizowapendeza, watoto wachanga wao mkawanyang'anya utukufu wangu, wasiupate kale na kale.
10
Kwa hiyo: Ondokeni! Nendeni! Kwani huku hakuna pa kutulia kwa ajili ya uchafu unaowaangamiza, mwangamie kabisa kabisa.
11
Kama angekuja mtu anayegeukageuka kama upepo, anayedanganya watu kwa kuwaongopea, kama angesema: Nitawahubiri mambo ya mvinyo na ya vileo, basi, yeye angekuwa mhubiri, watu hawa wanayemtaka.
12
Kweli nitawaokota nyote pia mlio wa Yakobo; kweli nitawakusanya mlio masao ya Isiraeli, niwaweke pamoja zizini kama kondoo, wawe kama kundi la kondoo walioko katikati ya malisho yao, wafanye mtutumo kwa kuwa watu wengi.
13
Mwenye kuwavunjia njia atawatangulia, wapite langoni kwa kupavunja, watoke nje papo hapo; ndipo, mfalme wao atakapowaongoza, lakini atakayekwenda mbele yao wote ni Bwana.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7