bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Micah 4
Micah 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 5 →
1
Mwisho wa siku utakapotimia, mlima wenye Nyumba ya Bwana utakuwa umeshikizwa na nguvu, uwe wa kwanza wa milima, uende juu kuliko vilima vingine; ndiko, makabila ya watu watakakokimbilia.
2
Nao wamizimu wengi watakwenda huko wakisema: Njoni, tupande mlimani kwa Bwana kwenye Nyumba ya Mungu wa Yakobo! Atufundishe, njia zake zilivyo, tupate kwenda na kuifuata mikondo yake! Kwani Maonyo yatatoka Sioni, namo Yerusalemu mtatoka Neno lake Bwana.
3
Ndipo, atakapoamulia makabila mengi na kuwapatiliza wamizimu wenye nguvu wakaao mbali; nao watazifua panga zao kuwa majembe, hata mikuki yao kuwa miundu, kwani hakuna taifa tena litakalochomolea jingine panga, wala hawatajifundisha tena mapigano ya vita.
4
Watakaa kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mkuyu wake pasipo kuona atakayewastusha, kwani kinywa cha Bwana Mwenye vikosi kimeyasema.
5
Kwani makabila yote kila moja hujiendea katika jina la mungu wake, lakini sisi tutakwenda kwa Jina la Bwana Mungu wetu siku zote kale na kale.
6
Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku hiyo nitawaokota wachechemeao, niwakusanye waliotawanyika nao niliowafanyizia mabaya.
7
Kisha nitawaweka wachechemeao kuwa masao, nao walioko mbali kuwa taifa lenye nguvu, naye Bwana atakuwa mfalme wao mlimani kwa Sioni toka sasa hata kale na kale.
8
Nawe mnara wa kulindia makundi, wewe kilima cha binti Sioni, kwako wewe utarudi tena, ukufikie, ule utawalaji wa kwanza, ndio ufalme wa binti Yerusalemu.
9
Mbona unapiga makelele sasa? Je? Mfalme hayumo mwako? Au ameangamia akuongozaye, uchungu ukikupata kama wa mwanamke anayezaa?
10
Jipinde na kupiga kite kama mwanamke anayezaa, binti Sioni! Kwani sasa huna budi kutoka mjini, ukae porini, mpaka ufike Babeli; huko ndiko, Bwana atakakokuponya akikukomboa mikononi mwa adui zako.
11
Lakini sasa wamizimu wengi watakukusanyikia wakisema: Sioni na uchafuliwe, macho yetu yaufurahie.
12
Lakini wao hawayajui mawazo ya Bwana, wala hawalitambui shauri lake, ya kuwa ni yeye aliyewakusanya kama miganda penye kupuria.
13
Inuka, binti Sioni, uwapure! Kwani pembe zako nitazigeuza kuwa chuma nayo kwato zako kuwa shaba, upate kuponda makabila mengi, umtolee Bwana mapato yao, yawe yake, nazo mali zao, ziwe zake yeye aliye Bwana wa nchi zote.
14
Sasa jikusanyeni, wana wa mkutano! Kwani wametujengea boma, watusonge, naye mwamuzi wa Isiraeli wanampiga shavuni kwa fimbo.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7