bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Micah 7
Micah 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
1
Yamenipata! Kwani yamenijia mambo yapatikanayo penye mwisho wa machumo ya matunda, siku za kiangazi zikitimia, au watu wakiokotezaokoteza zabibu: hakuna kichala cha zabibu za kula wala kuyu tu, roho yangu inazozitunukia sana.
2
Wamchao Mungu wametoweka katika nchi hii, kwa watu wa huku hakuna mwenye moyo unyokao. Wote huvizia, wamwage damu za watu, kila mmoja humtegea mwenziwe tanzi.
3
Kama ni kufanya mabaya, mikono yote miwili iko tayari, yamalizike vema. Mkuu ayatakayo, mwenye kukata mashauri huyafanya akipenyezewa mali; mwenye nguvu akiyasema, roho yake inayoyatamani, basi, yayo hayo wanayafunganyafunganya.
4
Aliye mwema kwao hufanana na mbigili, anyokaye moyo kwao ni mbaya kuliko boma la migunga. Siku, wapelelezi wako waliyoisema, ile siku, utakapopatilizwa, inakuja! Ndipo, watakapochafukwa na mioyo.
5
Usimtegemee mwenzio! Wala usimjetee rafiki yako umpendaye! Ilinde midomo ya kinywa chako, mwanamke alalaye kifuani pako asiyajue yaliyomo!
6
Kwani mwana wa kiume anambeza baba yake, naye mwana wa kike anamwinukia mama yake, vilevile mkwe na mkwewe, nao watakaomchukiza mtu ndio waliomo mwake.
7
Lakini mimi nitamchungulia Bwana, nimngojee Mungu wangu atakayeniokoa. Mungu wangu atanisikia.
8
Usinifurahie, uliye adui yangu! Kama ningeanguka, nitainuka tena. Kama ninakaa gizani, Bwana ni mwanga wangu.
9
Makali yake Bwana nitayavumilia, kwani nimemkosea: mwisho atanigombea magomvi yangu, anikatie shauri lililo sawa, atanitoa na kuniweka mwangani, nipate kuuona wongofu wake.
10
Naye adui yangu ataviona; ndipo, soni itakapomfunika, yeye aniulizaye sasa: Bwana Mungu wako yuko wapi? Macho yangu yatamfurahia, atakapokanyagwa kama taka ya barabarani.
11
Siku itakuja, kuta zako zitakapojengwa, siku hiyo mipaka yako itakuwa mbali.
12
Siku hiyo watakuja kwako watokao Asuri na miji ya Misri, tena kutoka Misri mpaka mto huo mkubwa, tena kutoka bahari hii mpaka bahari ya pili, tena kutoka mlima huu mpaka mlima ule.
13
Lakini kwanza nchi hii sharti iwe mapori tu kwa ajili yao waikaao; hayo ndiyo mapato ya matendo yao.
14
Walio ukoo wako wachunge kwa fimbo yako, ndilo kundi lililo fungu lako. ni wao wakaao peke yao katika mwitu huko Karmeli, walishe hata Basani na Gileadi kama siku za kale.
15
Kama siku zile, mlipotoka katika nchi ya Misri, nitawaonyesha mambo yatakayowastaajabisha.
16
Wamizimu watakapoyaona, watapatwa na soni, nguvu zao zote zikiwa za bure, wataweka mikono vinywani, nayo masikio watayaziba, yasisikie.
17
Watalamba mavumbi kama nyoka, kama wadudu watambaao chini watatoka mafichoni mwao na kutetemeka, wamjie Bwana Mungu wetu kwa kutishika, nawe wewe watakuogopa.
18
Je? Yuko Mungu afananaye na wewe, aondoaye maovu, ayapitaye mapotovu yao walio masao yao waliokuwa fungu lake? Hazishiki kale na kale nguvu za makali yake, kwani hupendezwa na kuwaendea watu kwa upole.
19
Nasi atatuhurumia tena, maovu yetu yote atayapondaponda, yatutoke, makosa yetu yote atayatupa vilindini mwa bahari.
20
Yakobo utamwendea kwa welekevu, naye Aburahamu kwa upole, kama ulivyowaapia baba zetu tangu siku zile za kale.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7