bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Micah 5
Micah 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 6 →
1
*Wewe Beti-Lehemu wa Efurata, ijapo uwe mdogo katika miji yenye maelfu ya Yuda, mwako ndimo, atakamonitokea yeye atakayekuwa mtawala Waisiraeli; matokeo yake ni ya siku nyingi za mbele, kweli ni ya siku za kale na kale.
2
Kwa hiyo atawatoa, siku zitimie, yule atakayezaa atakapokuwa amezaa; ndipo, wazao wa ndugu zao watakaporudi kwao kwa wana wa Isiraeli.
3
Ndipo, atakapotokea na kusimama, awachunge kwa nguvu za Bwana, kwa ukuu wa Jina la Bwana Mungu wake, nao watakaa, kwani hapo ndipo, atakapokua, awe mkuu mpaka mapeoni kwa nchi.
4
Naye yeye atakuwa utengemano wetu.* Kama Waasuri wataingia katika nchi yetu, wakanyage namo majumbani mwetu, tutaweka wachungaji wetu saba, wawazuie, pamoja na watu wanane wa kifalme.
5
Hao watailisha nchi ya Asuri kwa panga nayo nchi ya Nimurodi malangoni kwake. Ndivyo, atakavyotuponya mikononi mwa Waasuri, kama wanaingia katika nchi yetu na kukanyaga mipakani kwetu.
6
Nao masao ya Isiraeli watakuwa kati ya makabila mengi kama umande utokao kwa Bwana, au kama manyunyu yanyeayo majani yasiyomngojea mtu, yasiyokalii wana wa watu.
7
Kweli masao ya Yakobo watakuwa kwa wamizimu kati ya makabila mengi, kama simba alivyo katika nyama wa porini, au kama mwana wa simba alivyo katika makundi ya kondoo, akiwapita huwakanyaga pamoja na kuwararua, asipatikane mponya.
8
Hivyo mkono wako utakuwa mkuu kwao wakusongao, nao adui zako watatoweshwa wote.
9
Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku hiyo itakuwa, nitakapotowesha kwako farasi wako, nayo magari yako ya vita nitayapoteza.
10
Nayo miji ya nchi yako nitaitowesha, nayo maboma yako yote nitayabomoa.
11
Nazo hirizi nitazitowesha mikononi pako, nao waaguaji hawatakuwako kwako.
12
Tena ndipo, nitakapovitowesha kwako vinyago vyako na nguzo zako za mawe za kutambikia, usiangukie tena yaliyo kazi za mikono yako.
13
Hata mifano yenu ya mwezi nitaing'oa kwako, nayo miji yako nitaiangamiza.
14
Kwa makali yenye moto nitawalipisha wamizimu wasiosikia.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7