bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Jeremiah 14
Jeremiah 14
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 15 →
1
Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia kuhusu ule ukame:
2
“Watu wa Yuda wanaomboleza, na malango yao yanalegea. Watu wake wanaomboleza udongoni na kilio cha Yerusalemu kinapanda juu.
3
Wakuu wake wanawatuma watumishi wao maji; watumishi wanakwenda visimani, lakini maji hawapati; wanarudi na vyombo vitupu. Kwa aibu na fadhaa wanafunika vichwa vyao.
4
Wakulima wanahuzunika na kufunika vichwa vyao kwa kuona jinsi ardhi ilivyonyauka.
5
Hata kulungu porini anamwacha mtoto wake mchanga, kwa sababu hakuna nyasi.
6
Pundamwitu wanasimama juu ya vilele vikavu, wanatweta kwa kukosa hewa kama mbweha; macho yao yanafifia kwa kukosa chakula.
7
“Nao watu wanasema: Ingawa dhambi zetu zashuhudia dhidi yetu, utusaidie ee Mwenyezi-Mungu kwa heshima ya jina lako. Maasi yetu ni mengi, tumetenda dhambi dhidi yako.
8
Ewe uliye tumaini la Israeli, mwokozi wetu wakati wa taabu, utakuwaje kama mgeni nchini mwetu, kama msafiri alalaye usiku mmoja?
9
Utakuwaje kama mtu uliyechanganyikiwa, kama shujaa asiyeweza kusaidia mtu? Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, u pamoja nasi; sisi twaitwa kwa jina lako, usituache.”
10
Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya watu hawa: “Kweli wamependa sana kutangatanga, wala hawakujizuia; kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu siwapokei. Sasa nitayakumbuka makosa yao, na kuwaadhibu kwa dhambi zao.”
11
Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Usiwaombee watu hawa fanaka.
12
Hata wakifunga, sitayasikiliza maombi yao, na hata wakinitolea sadaka za kuteketeza na za nafaka, mimi sitazikubali. Bali nitawaangamiza kwa upanga, njaa na tauni.”
13
Kisha mimi nikasema, “Tazama, ee Bwana Mwenyezi-Mungu! Manabii wanawaambia watu hawa kwamba hapatakuwa na vita wala njaa, kwa sababu umeahidi kuwa patakuwa na amani tu katika nchi yetu.”
14
Naye Mwenyezi-Mungu, akaniambia: “Hao manabii wanatoa unabii wa uongo kwa jina langu. Mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, maaguzi yasiyo na maana yoyote, uongo wanaojitungia wenyewe.
15
Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi kuhusu hao manabii wanaotabiri kwa jina langu, ingawa mimi sikuwatuma, na wanaosema kwamba hapatakuwa na vita wala njaa katika nchi hii: Manabii hao wataangamia kwa upanga na kwa njaa.
16
Na hao ambao waliwatabiria mambo hayo, watatupwa nje katika barabara za Yerusalemu wakiwa wamekufa kwa njaa na vita, wala hapatakuwa na mtu wa kuwazika. Hayo yatawapata wao wenyewe, wake zao, watoto wao wa kike na wa kiume; maana mimi nitawamwagia uovu wao wenyewe.
17
Hivi ndivyo utakavyowaambia: Laiti macho yangetoa machozi kutwa kucha, wala yasikome kububujika, maana, watu wangu wamejeruhiwa vibaya, wamepata pigo kubwa sana.
18
Nikienda nje mashambani, naiona miili ya waliouawa vitani; nikiingia ndani ya mji, naona tu waliokufa kwa njaa! Manabii na makuhani wanashughulikia mambo yao nchini, wala hawajui wanalofanya.”
19
Ee Mwenyezi-Mungu, je, umemkataa Yuda kabisa? Je, moyo wako umechukizwa na Siyoni? Kwa nini umetupiga vibaya, hata hatuwezi kupona tena? Tulitazamia amani, lakini hatukupata jema lolote; tulitazamia wakati wa kuponywa, badala yake tukapata vitisho.
20
Tunakiri uovu wetu, ee Mwenyezi-Mungu, tunakiri uovu wa wazee wetu, maana, tumekukosea wewe.
21
Usitutupe, kwa heshima ya jina lako; usikidharau kiti chako cha enzi kitukufu. Ukumbuke agano ulilofanya nasi, wala usilivunje.
22
Je miungu ya uongo ya mataifa yaweza kuleta mvua? Au, je, mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je, si wewe ee Mwenyezi-Mungu uliye Mungu wetu? Tunakuwekea wewe tumaini letu, maana wewe unayafanya haya yote.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52