bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Jeremiah 5
Jeremiah 5
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 6 →
1
Kimbieni huko na huko mjini Yerusalemu; pelelezeni na kujionea wenyewe! Chunguzeni masoko yake mwone kama kuna mtu atendaye haki mtu atafutaye ukweli; akiwako, basi Mwenyezi-Mungu atausamehe Yerusalemu.
2
Ingawa wanaapa: “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo”, viapo vyao ni vya uongo.
3
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe watafuta daima uaminifu. Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu; umewateketeza, lakini walikataa kukosolewa. Wamezifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba; wamekataa kabisa kurudi kwako.
4
Ndipo nilipowaza: “Hawa ni watu duni hawana akili; hawajui matakwa ya Mwenyezi-Mungu, hawajui Sheria ya Mungu wao.
5
Nitawaendea wakuu niongee nao; bila shaka, wao wanajua matakwa ya Mwenyezi-Mungu; wanajua sheria ya Mungu wao.” Lakini wote waliivunja nira yao. Waliikatilia mbali minyororo yao.
6
Kwa hiyo simba kutoka msituni atawaua; mbwamwitu kutoka jangwani atawararua. Chui anaivizia miji yao. Kila atokaye humo atararuliwa vipandevipande, kwa sababu dhambi zao ni nyingi, maasi yao ni makubwa.
7
Mwenyezi-Mungu anauliza: “Nitawezaje kukusamehe ee Yerusalemu? Watu wako wameniasi; wameapa kwa miungu ya uongo. Nilipowashibisha kwa chakula, wao walifanya uzinzi, wakajumuika majumbani mwa makahaba.
8
Walikuwa kama farasi walioshiba wenye tamaa, kila mmoja akimtamani mke wa jirani yake.
9
Je, nisiwaadhibu kwa mambo haya yote? Nisilipize kisasi juu ya taifa kama hili?
10
“Pandeni mpite katika mashamba yake ya mizabibu mkaharibu kila kitu bila kumaliza kabisa. Yakateni matawi yake, kwani hayo si yangu mimi Mwenyezi-Mungu.
11
Naam, watu wa Israeli na watu wa Yuda, wamekosa kabisa uaminifu kwangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
12
Wamesema uongo juu ya Mwenyezi-Mungu wamesema: “Hatafanya kitu; hatutapatwa na uovu wowote; hatutashambuliwa wala kuona njaa.
13
Manabii si kitu, ni upepo tu; maana neno lake Mungu halimo ndani yao.” Basi hayo na yawapate wao wenyewe!
14
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Kwa kuwa wao wamesema jambo hilo, sasa nitayafanya maneno niliyokupa wewe Yeremia kuwa moto. Watu hawa watakuwa kuni, na moto huo utawateketeza.
15
“Nami Mwenyezi-Mungu nasema juu yenu enyi Waisraeli: Mimi naleta taifa moja kutoka mbali, lije kuwashambulia. Taifa ambalo halishindiki, taifa ambalo ni la zamani, ambalo lugha yake hamuifahamu, wala hamwezi kuelewa wasemacho.
16
Mishale yao husambaza kifo; wote ni mashujaa wa vita.
17
Watayala mazao yenu na chakula chenu; watawamaliza watoto wenu wa kike na wa kiume. Watachinja makundi yenu ya kondoo na ng'ombe; wataiharibu mizabibu yenu na mitini yenu. Miji yenu ya ngome mnayoitegemea, wataiharibu kwa silaha zao.
18
“Lakini, hata katika siku hizo mimi Mwenyezi-Mungu nasema, sitawaangamiza na kuwamaliza kabisa.
19
Na watu wenu watakapouliza ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametutendea mambo hayo yote?’ Wewe utawaambia, ‘Nyinyi mlimwacha Mwenyezi-Mungu, mkaitumikia miungu ya kigeni katika nchi yenu. Basi ndivyo mtakavyowatumikia watu wengine katika nchi isiyo yenu.’
20
“Watangazie wazawa wa Yakobo, waambie watu wa Yuda hivi:
21
Sikilizeni enyi wajinga na wapumbavu; watu mlio na macho, lakini hamwoni, mlio na masikio, lakini hamsikii.
22
Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu! Kwa nini hamtetemeki mbele yangu? Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari, kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.
23
Lakini watu hawa wana moyo wa ukaidi na uasi; wameniacha wakaenda zao.
24
Wala hawasemi mioyoni mwao; ‘Na tumche Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, anayetujalia mvua kwa wakati wake, anayetupatia mvua za masika na mvua za vuli; na kutupa majira maalumu ya mavuno.’
25
Makosa yenu yamewazuia msipate baraka hizo, dhambi zenu zimewafanya msipate mema.
26
Naam, kuna walaghai miongoni mwa watu wangu, watu ambao hunyakua mali za wengine. Wako kama wawindaji wa ndege: Hutega mitego yao na kuwanasa watu.
27
Kama vile kapu lililojaa ndege walionaswa, ndivyo nyumba zao zilivyojaa mali za udanganyifu. Ndiyo maana wamekuwa watu wakubwa na matajiri,
28
wamenenepa na kunawiri. Katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa haki wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za watu maskini.
29
“Je, nisiwaadhibu kwa mambo haya? Je nitaacha kulipiza kisasi taifa kama hili?
30
Jambo la ajabu na la kuchukiza limetokea katika nchi hii:
31
Manabii wanatabiri mambo ya uongo, makuhani nao hutafuta faida yao wenyewe; na watu wangu wanaona jambo hilo kuwa sawa. Lakini mwisho utakapofika mtafanyaje?”
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52