bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Jeremiah 28
Jeremiah 28
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 29 →
1
Mwaka uleule, mnamo mwezi wa tano wa mwaka wa nne wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, Hanania mwana wa Azuri, nabii kutoka mji wa Gibeoni, alisema nami katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Alisema nami mbele ya makuhani na watu wote, akaniambia,
2
“Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Nimeivunja nira ya mfalme wa Babuloni.
3
Mnamo miaka miwili nitavirudisha hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babuloni alivichukua na kuvipeleka Babuloni.
4
Pia nitamrudisha Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na watu wote wa Yuda waliohamishiwa Babuloni. Naam, nitaivunja nira ya mfalme wa Babuloni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
5
Kisha, nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania mbele ya makuhani na watu wote waliokuwa wamesimama katika hekalu la Mwenyezi-Mungu:
6
“Na iwe hivyo! Mwenyezi-Mungu na afanye hivyo. Mwenyezi-Mungu na ayatimize maneno uliyotabiri, avirudishe hapa vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoka Babuloni pamoja na watu wote waliohamishiwa huko.
7
Lakini sikiliza neno ninalokuambia wewe na watu wote.
8
Manabii waliotutangulia mimi na wewe, tangu zamani za kale, walitabiri kwamba vita, njaa na maradhi vitazikumba nchi nyingi na tawala kubwa.
9
Lakini nabii atabiriye amani, hutambuliwa tu kama nabii aliyetumwa na Mwenyezi-Mungu, ikiwa mambo aliyotabiri hutokea kweli.”
10
Ndipo nabii Hanania akaichukua ile nira shingoni mwa nabii Yeremia, akaivunja.
11
Naye Hanania akasema hivi mbele ya watu wote, “Mwenyezi-Mungu asema: Hivi ndivyo nitakavyovunja nira ambayo mfalme Nebukadneza ameyavisha mataifa yote; nitafanya hivyo mnamo miaka miwili ijayo.” Kisha nabii Yeremia akaenda zake.
12
Baada ya nabii Hanania kuvunja nira kutoka shingoni mwa nabii Yeremia, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia:
13
“Nenda ukamwambie Hanania kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wewe umevunja nira ya mti, lakini mimi nitatengeneza nyingine ya chuma.
14
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema kuwa nimeweka nira ya chuma ya utumwa shingoni mwa mataifa haya yote, nayo yatamtumikia Nebukadneza, mfalme wa Babuloni. Nimempa Nebukadneza hata wanyama wa porini wamtumikie.”
15
Basi, nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza, Hanania, Mwenyezi-Mungu hakukutuma, nawe unawafanya watu hawa waamini uongo.
16
Kwa hiyo Mwenyezi-Mungu asema kwamba atakuondoa duniani. Mwaka huuhuu utakufa, kwa sababu umewaambia watu wamwasi Mwenyezi-Mungu.”
17
Mwaka huohuo, mnamo mwezi wa saba, nabii Hanania akafa.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52