bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Jeremiah 46
Jeremiah 46
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 45
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 47 →
1
Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia Yeremia kuhusu watu wa mataifa.
2
Kuhusu Misri na jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililokuwa huko Karkemishi karibu na mto Eufrate ambalo Nebukadneza mfalme wa Babuloni alilishambulia mnamo mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:
3
Tayarisheni ngao ndogo na kubwa msonge mbele kupigana vita.
4
Tandikeni farasi na kuwapanda, Shikeni nafasi zenu na kofia za chuma mvae. Noeni mikuki yenu, vaeni mavazi yenu ya chuma!
5
Lakini mbona nawaona wametishwa? Wamerudi nyuma. Mashujaa wao wamepigwa, wamekimbia mbio, bila hata kugeuka nyuma. Kitisho kila upande. Mwenyezi-Mungu amesema.
6
Walio wepesi kutoroka hawawezi, mashujaa hawawezi kukwepa; huko kaskazini kwenye mto Eufrate wamejikwaa na kuanguka.
7
Nani huyo aliye kama mto Nili uliofurika kama mito inayoumuka mawimbi?
8
Misri ni kama mto Nili uliofurika kama mito inayoumuka mawimbi Ilisema: “Nitajaa, nitaifunika nchi, nitaiharibu miji na wakazi wake.
9
Songeni mbele, enyi farasi, shambulieni enyi magari ya farasi. Mashujaa wasonge mbele: Watu wa Kushi na Puti washikao ngao, watu wa Ludi, stadi wa kutumia pinde.”
10
Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ni siku ya kulipiza kisasi; naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utainywa damu yao na kushiba. Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafara huko kaskazini karibu na mto Eufrate.
11
Pandeni Gileadi, enyi watu wa Misri, mkachukue dawa ya marhamu. Mmetumia dawa nyingi bure; hakuna kitakachowaponya nyinyi.
12
Mataifa yamesikia aibu yenu, kilio chenu kimeenea duniani kote; mashujaa wamegongana wenyewe kwa wenyewe, wote pamoja wameanguka.
13
Neno ambalo Mwenyezi-Mungu alimwambia Yeremia wakati alipofika Nebukadneza mfalme wa Babuloni kuishambulia nchi ya Misri:
14
“Tangaza nchini Misri, piga mbiu huko Migdoli, tangaza huko Memfisi na Tahpanesi. Waambie: ‘Kaeni tayari kabisa maana upanga utawaangamiza kila mahali.’
15
Kwa nini shujaa wako amekimbia? Mbona fahali wako hakuweza kustahimili? Kwa sababu mimi Mwenyezi-Mungu nilimwangusha chini!
16
Wengi walijikwaa, wakaanguka, kisha wakaambiana wao kwa wao: ‘Simameni, tuwaendee watu wetu, turudi katika nchi yetu, tuukimbie upanga wa adui.’
17
“Naye Farao, mfalme wa Misri, mpangeni jina hili: ‘Kishindo kitupu!’
18
Mimi naapa kwa uhai wangu nasema mimi mfalme niitwaye Mwenyezi-Mungu wa majeshi, kweli adui anakuja kuwashambulieni: Ni hakika kama Tabori ulivyo mlima kama mlima Karmeli uonekanavyo kutoka baharini.
19
Enyi wakazi wa Misri jitayarisheni na mizigo kwenda uhamishoni! Maana mji wa Memfisi utaharibiwa kabisa, utakuwa magofu yasiyokaliwa na watu.
20
Misri ni kama mtamba mzuri wa ng'ombe, lakini kipanga kutoka kaskazini amemvamia.
21
Hata askari wake wa kukodiwa ni kama ndama wanono; nao pia wamegeuka, wakakimbia pamoja, wala hawakuweza kustahimili, kwa maana siku yao ya kuangamizwa imefika, wakati wao wa kuadhibiwa umewadia.
22
Misri anatoa sauti kama nyoka anayekimbia; maana maadui zake wanamjia kwa nguvu, wanamjia kwa mashoka kama wakata-miti.
23
Wataukata kabisa msitu wake, ingawa haupenyeki, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, maana wao ni wengi kuliko nzige wasiohesabika.
24
Watu wa Misri wataaibishwa, watatiwa mikononi mwa watu kutoka kaskazini.”
25
Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, alisema: “Tazama, mimi nitamwadhibu Amoni mungu wa Thebesi, nitaiadhibu Misri na miungu yake na wafalme wake, nitamwadhibu Farao na wote wanaomtegemea.
26
Nitawatia mikononi mwa wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babuloni na maofisa wake. Baadaye, nchi ya Misri itakaliwa na watu kama ilivyokuwa hapo zamani. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
27
“Lakini wewe usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli; maana, kutoka mbali nitakuokoa, nitakuja kuwaokoa wazawa wako kutoka nchi walimohamishwa. Yakobo utarudi na kutulia na kustarehe, wala hakuna yeyote atakayekutia hofu.
28
Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, kwa maana mimi niko pamoja nawe. Nitayaangamiza kabisa mataifa yote ambayo nimekutawanya kati yao, lakini wewe sitakuangamiza. Nitakuchapa kadiri unavyostahili, sitakuacha bila kukuadhibu.”
← Chapter 45
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 47 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52