bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Jeremiah 19
Jeremiah 19
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 20 →
1
Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kwa mfinyanzi. Kisha, wachukue baadhi ya wazee wa watu na baadhi ya makuhani viongozi,
2
halafu uende pamoja nao katika bonde la Mwana wa Hinomu, kwa kupitia lango la Vigae. Ukifika huko, tangaza maneno ninayokuambia.
3
Utasema hivi: Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu enyi wafalme wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Kweli ninaleta maafa mabaya mahali hapa, hata kila mmoja atakayesikia habari zake, atapigwa na bumbuazi.
4
Kwa maana watu wameniacha mimi na kupatia unajisi mahali hapa kwa kufukizia ubani miungu mingine; miungu ambayo wao wenyewe, wazee wao wala wafalme wa Yuda hawajapata kuijua. Pia wamepajaza mahali hapa damu ya watu wasio na hatia,
5
wakamjengea mungu Baali madhabahu, ili kuwachoma wana wao kama sadaka ya kuteketezwa. Mimi sijapata kuamuru wala kuagiza jambo kama hilo lifanywe, wala hata sijapata kulifikiria.
6
Kwa hiyo, jueni kuwa siku zaja ambapo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala bonde la Mwana wa Hinomu, bali pataitwa bonde la Mauaji. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
7
Na papa hapa nitaivuruga mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya watu wao washindwe na kuuawa na maadui zao vitani na kuangamizwa na wale wanaowawinda. Maiti zao nitawaachia ndege wa anga na wanyama wa porini kuwa chakula chao.
8
Nitaufanya mji huu kuwa mahali pa kushangaza; naam, nitaufanya uwe kitu cha kuzomewa. Kila mtu anayepita karibu nao atashangaa na kuuzomea kwa sababu ya maafa yote yatakayoupata.
9
Maadui watauzingira na kujaribu kuwaua watu wake. Watasababisha hali mbaya sana mjini humo hata watu watawala watoto wao wa kike na wa kiume, na kila mtu atamla mwenzake.
10
Kisha wewe utalivunja gudulia hilo mbele ya watu hao watakaokwenda pamoja nawe,
11
na kuwaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema hivi: Ndivyo nitakavyovunjavunja watu hawa na mji huu kama vile mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, hata kisiweze kamwe kutengenezwa tena. Watu watazikwa Tofethi, kwa sababu hapatakuwa na mahali pengine pa kuzikia.
12
Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa na wakazi wake; nitaufanya mji huu kama Tofethi.
13
Nyumba za Yerusalemu na ikulu za wafalme wa Yuda, naam, nyumba zote ambazo juu ya paa zake watu walifukiza ubani kwa sayari za mbinguni, na kumiminia miungu mingine tambiko za divai, zote zitatiwa unajisi kama Tofethi.”
14
Baada ya hayo, Yeremia aliondoka Tofethi, mahali ambako Mwenyezi-Mungu alimtuma aende kutoa unabii, akaenda na kusimama katika ukumbi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, akawatangazia watu wote akisema:
15
“Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, mimi nitauletea mji huu na vijiji vyote vilivyo jirani maafa yote niliyoutangazia, kwa sababu wakazi wake ni wakaidi na wamekataa kusikia maneno yangu.”
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52