bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Jeremiah 8
Jeremiah 8
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 9 →
1
“Wakati huo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, mifupa ya wafalme wa Yuda, mifupa ya wakuu wao, mifupa ya makuhani, mifupa ya manabii na mifupa ya wakazi wote wa Yerusalemu itachimbuliwa makaburini mwao.
2
Itaachwa imetandazwa mbele ya jua na mwezi na sayari zote za mbinguni, vitu ambavyo walivipenda na kuvitumikia, wakavitaka shauri na kuviabudu. Mifupa hiyo haitakusanywa wala kuzikwa, bali itakuwa kama mavi juu ya ardhi.
3
Watu wote waliobaki wa jamaa hii mbovu, mahali popote pale nilipowatawanya, wataona heri kufa kuliko kuishi. Ndivyo nisemavyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
4
“Wewe Yeremia utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mtu akianguka, je hainuki tena? Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?
5
Mbona basi, watu hawa wameacha njia iliyo sawa na kuendelea katika upotovu wao? Wanashikilia miungu yao ya uongo, na kukataa kunirudia mimi!
6
Mimi nilisikiliza kwa makini, lakini wao hawakusema ukweli wowote. Hakuna mtu anayetubu uovu wake, wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’ Kila mmoja wao anashika njia yake, kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.
7
Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbayuwayu na koikoi, hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawa hawajui kitu juu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.
8
Mnawezaje kusema: ‘Sisi tuna hekima, sisi tunayo sheria ya Mwenyezi-Mungu,’ hali waandishi wa sheria, wameipotosha sheria yangu?
9
Wenye hekima wenu wataaibishwa; watafadhaishwa na kunaswa. Wamelikataa neno la Mwenyezi-Mungu; je, ni hekima gani hiyo waliyo nayo?
10
Kwa hiyo, wake zao nitawapa watu wengine, mashamba yao nitawapa wengine. Maana, tangu mdogo hadi mkubwa, kila mmoja ana tamaa ya faida haramu. Tangu manabii hadi makuhani, kila mmoja anatenda kwa udanganyifu.
11
Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu, wakisema, ‘Kuna amani, kuna amani’, kumbe hakuna amani yoyote!
12
Je, waliona aibu walipotenda machukizo hayo? La hasha! Hawakuona aibu hata kidogo. Hata hawajui kuona haya. Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka; nitakapowaadhibu, wataangamia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
13
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao, sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu, sikupata tini zozote juu ya mtini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”
14
“Watu wanauliza: Kwa nini sisi tunakaa tu hapa? Kusanyikeni, tuingie katika miji yenye ngome, tukaangamie huko! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupangia tuangamie, ametupa maji yenye sumu tunywe, kwa kuwa tumemkosea yeye.
15
Tulitazamia kupata amani, lakini hakuna jema lililotokea. Tulitazamia wakati wa kuponywa, badala yake tukapata vitisho.
16
Sauti za farasi wao zinasikika, kwa mlio wa farasi wao wa vita, nchi nzima inatetemeka. Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo, kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.
17
“Basi nitawaleteeni nyoka; nyoka wenye sumu wasioweza kurogwa na walozi, nao watawauma nyinyi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
18
Huzuni yangu haiwezi kutulizwa, moyo wangu wasononeka ndani yangu.
19
Sikiliza kilio cha watu wangu, kutoka kila upande katika nchi. “Je, Mwenyezi-Mungu hayuko Siyoni? Je, mfalme wake hayuko tena huko?” “Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao za miungu, na vinyago vyao vya miungu ya kigeni?”
20
“Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, nasi bado hatujaokolewa!
21
Jeraha la watu wangu limeniumiza moyoni, ninaomboleza na kufadhaika.
22
Je, hakuna dawa ya kupaka huko Gileadi? Je, hakuna mganga huko? Mbona basi watu wangu hawajaponywa?
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52