bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Jeremiah 18
Jeremiah 18
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 19 →
1
Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2
“Yeremia, inuka uende nyumbani kwa mfinyanzi, na huko nitakupa maneno yangu.”
3
Basi, nikateremka mpaka nyumbani kwa mfinyanzi, nikamkuta mfinyanzi akifanya kazi yake penye gurudumu la kufinyangia.
4
Na ikawa kwamba chombo alichokifinyanga kilipoharibika mikononi mwake, yeye alifinyanga upya chombo kingine kadiri ilivyompendeza.
5
Kisha, neno la Mwenyezi-Mungu likanijia:
6
“Enyi Waisraeli! Je, mimi Mwenyezi-Mungu siwezi kuwafanya nyinyi kama alivyofanya mfinyanzi huyu? Jueni kuwa kama ulivyo udongo mikononi mwa mfinyanzi, ndivyo nyinyi mlivyo mikononi mwangu.
7
Wakati wowote nitakapotoa tamko kuhusu taifa au ufalme kwamba nitalingoa na kulivunja na kuliangamiza,
8
halafu taifa hilo likageuka na kuacha uovu wake, basi, mimi nitaacha kulitendea yale mambo niliyokusudia kulitendea.
9
Hali kadhalika, wakati wowote nikitoa tamko kuhusu taifa au ufalme kwamba nitalijenga na kulistawisha,
10
kisha taifa hilo likafanya uovu mbele yangu na kukataa kunitii, basi, mimi nitaacha kulitendea mema hayo niliyokusudia kulitendea.
11
Sasa, basi, waambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi Hufinyanga jambo ovu dhidi yenu na kufanya mpango dhidi yenu. Rudini na kuacha njia zenu mbaya, mkarekebishe mienendo yenu na matendo yenu.
12
Lakini wao watasema, ‘Hiyo ni bure tu! Tutafuata mipango yetu wenyewe na kila mmoja wetu atafanya kwa kiburi kadiri ya moyo wake mwovu.’”
13
Basi, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Yaulize mataifa yote: Nani amewahi kusikia jambo kama hili. Israeli amefanya jambo la kuchukiza mno.
14
Je, majabali ya Lebanoni hukosa theluji? Je, vijito vya maji vya milima yake hukauka?
15
Lakini watu wangu wamenisahau mimi, wanafukizia ubani miungu ya uongo. Wamejikwaa katika njia zao, katika barabara za zamani. Wanapitia vichochoroni badala ya njia kuu.
16
Wameifanya nchi yao kuwa kitisho, kitu cha kuzomewa daima. Kila mtu apitaye huko hushangaa na kutikisa kichwa chake.
17
Nitawatawanya mbele ya adui, kama upepo utokao mashariki. Nitawapa kisogo badala ya kuwaonesha uso wangu siku hiyo ya kupata maafa yao.”
18
Kisha, watu wakasema: “Njoni tumfanyie Yeremia njama, maana hatukosi makuhani wa kutufundisha, wenye hekima wa kutushauri na manabii wa kututangazia ujumbe wa Mungu! Njoni tumshtaki kwa maneno yake mwenyewe, wala tusiyatilie maanani yote asemayo.”
19
Basi, mimi nikasali: Nitegee sikio ee Mwenyezi-Mungu, usikilize ombi langu.
20
Je, mtu hulipwa mabaya kwa mema? Walakini, wamenichimbia shimo. Kumbuka nilivyosimama mbele yako, nikasema mema kwa ajili yao, ili kuiepusha hasira yako mbali nao.
21
Kwa hiyo waache watoto wao wafe njaa, waache wafe vitani kwa upanga. Wake zao wawe tasa na wajane. Waume zao wafe kwa maradhi mabaya na vijana wao wachinjwe kwa upanga vitani.
22
Kilio na kisikike majumbani mwao, unapowaletea kundi la wanyanganyi ghafla. Maana wamechimba shimo waninase; wameitegea mitego miguu yangu.
23
Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wazijua njama zao zote za kuniua. Usiwasamehe uovu wao, wala kufuta dhambi zao. Waanguke chini mbele yako; uwakabili wakati wa hasira yako.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52