bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Zechariah 10
Zechariah 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 11 →
1
Mwombeni Bwana mvua siku za vuli! Bwana ndiye afanye mawingu yenye umeme; naye ndiye anayewapa matone ya mvua, majani yote ya shambani yaipate.
2
Kwani vinyago husema yasiyo na maana, nao waaguaji huona yaliyo uwongo, husema ndoto zisizo za kweli, wakituliza mioyo, ni bure; kwa hiyo watu hujiendea kama kondoo, huteseka, kwani hakuna awachungaye.
3
Wachungaji ndio, makali yangu yanaowawakia moto, nao viongozi ndio, nitakaowapatiliza; kwani Bwana Mwenye vikosi amelikagua kundi lake, ndio mlango wa Yuda, nao ndio atakaowageuza, wawe kama farasi mwenye utukufu wake katika mapigano.
4
Kwao ndiko, kutakakotoka jiwe la pembeni, hata uwambo wa hema, hata upindi wa kupigania, kweli kwao ndiko, watakakotokea wote pia waongozao vikosi.
5
Nao watakuwa kama mafundi wa vita, wawakanyagao adui matopeni barabarani kwenye mapigano; watakapopigana, Bwana atakuwa nao, wawatweze waliopanda farasi.
6
Nitawatia nguvu walio mlango wa Yuda, nao walio mlango wa Yosefu nitawaokoa, nitawarudisha kwao, kwani nitawahurumia, nao watakuwa kama watu, nisiowatupa kwani mimi Bwana ni Mungu wao, nami nitawaitikia.
7
Nao Waefuraimu watakuwa kama mafundi wa vita, nayo mioyo yao itafurahiwa kama yao waliokunywa mvinyo; wana wao watakapoyaona, watafurahi, nayo mioyo yao itashangilia kwa kuwa na Bwana.
8
Nitawakusanya na kuwapigia miluzi, kwani nitawakomboa; nao watakuwa wengi, kama walivyokuwa wengi kale.
9
Nimewatawanya katika makabila mengine, lakini huko mbali nako watanikumbuka; kwa hiyo watapona pamoja na wana wao, wapate kurudi kwao.
10
Nami nitawarudisha kwao na kuwatoa katika nchi ya Misri, nitawakusanya na kuwatoa katika nchi ya Asuri, niwapeleke katika nchi ya Gileadi na ya Libanoni, lakini huko nako hawataenea wote.
11
Watakapopita baharini penye masongano, atayapiga mawimbi pale baharini; ndipo, mafuriko ya maji ya jito la Nili yatakapokupwa yote, nayo majivuno ya Asuri yatanyenyekezwa, nayo bakora ya kifalme ya Misri haitakuwa na budi kutoweka.
12
Nami nitawatia nguvu za kuwa na Bwana, wafanye mwenendo wao katika Jina lake; ndivyo, asemavyo Bwana.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14