bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Zechariah 9
Zechariah 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 10 →
1
Hili ndilo tamko zito la Bwana. linaionya nchi ya Hadiraki na mji wa Damasko, lipate kutua humo, kwani Bwana ndiye, watu wanayemwelekezea macho pamoja na koo zote za Isiraeli.
2
Linaionya nchi ya Hamati inayopakana nao, hata Tiro na Sidoni, kwani ni yenye werevu mwingi ulio wa kweli:
3
Watiro walijijengea boma, wakalimbika fedha, kama ni mavumbi, na dhahabu tupu kama ni taka za barabarani.
4
Lakini mtaona, Bwana akiuteka, azibwage mali zake pamoja na vikosi vyake baharini, lakini wenyewe utateketezwa kwa moto.
5
Askaloni utakapoyaona, utashikwa na woga; nao Gaza utatetemeka sana, Ekroni nao, kwa kuwa mji huo, walioungojea, utakuwa umewatia soni; namo Gaza mfalme atatoweka namo Askaloni hawatakaa watu tena.
6
Asdodi watakaa wana wa ugoni, lakini nitayakomesha majivuno ya Wafilisti.
7
Tena nitaziondoa nyama zao zenye damu vinywani mwao, navyo vyakula vyao vitapishavyo nitaviondoa katika meno yao; ndipo, nao walio masao yao watakapomjua Mungu wetu, wawe kama mkuu kwao Wayuda, nao Waekroni wawe kama Wayebusi.
8
*Kisha nitapiga kambi, iwe kilindo cha Nyumba yangu, pasipite mtu kwenda na kurudi, wala pasipite kwao tena mtesaji, kwani tangu hapo nitawaangalia kwa macho yangu,
9
Piga vigelegele sana, binti Sioni! Shangilia, binti Yerusalemu! Tazama, mfalme wako anakujia! Ni mwongofu na mwokozi, tena ni mnyenyekevu, amepanda punda aliye mwana bado wa kuwa na mama yake.
10
Ndipo, nitakapoyatowesha magari kule Efuraimu, nao farasi mle Yerusalemu, nazo pindi za vita zitatoweshwa, nao wamizimu atawafundisha kutengemana; ufalme wake utaanzia baharini, uifikie bahari ya pili, tena uanzie penye jito kubwa, uyafikie mapeo ya nchi.
11
Wafungwa wako wewe nitawakomboa kwa ajili ya damu ya agano lako, niwatoe shimoni msimo na maji.
12
Rudini ngomeni, ninyi wafungwa mliokishika kingojeo chenu! Leo hivi nawaambia: Nitakurudishia mara mbili yaliyokuwa yako.*
13
Kwani Wayuda ninawatumia kuwa upindi wangu, nao Waefuraimu kuwa mishale; kisha nitawaamsha wanao, Sioni, wawaendee wana wako, Ugriki; ndipo, nitakapokugeuza kuwa kama upanga wa fundi wa vita
14
Naye Bwana ataoneka kwao, mshale wake utokee kama umeme; kisha Bwana Mungu atapiga baragumu akija katika pepo kali za nchi ya kusini.
15
Bwana Mwenye vikosi atawakingia kwa ngao yake, waje kuwala wakiyakanyaga mawe ya makombeo, watakunywa damu zao wakipiga makelele kama wanaokunywa mvinyo; hivyo watajaa kama mabakuli yachukuayo damu za ng'ombe za tambiko, hivyo wenyewe watakuwa kama pembe za meza ya kutambikia.
16
Ndivyo, Bwana Mungu wao atakavyowaokoa siku hiyo, kwa kuwa ndio kundi lao walio ukoo wake, tena ndio vito vya taji vinavyometameta katika nchi yake.
17
Tazameni, wema wao na uzuri wao ulivyokuwa mwingi! Ngano hukuza vijana wa kiume nazo pombe mbichi vijana wa kike.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14