bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Zechariah 7
Zechariah 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 8 →
1
Katika mwaka wa nne wa mfalme Dario ndipo, neno la Bwana lilipomjia Zakaria siku ya nne ya mwezi wa Kisilewu ulio wa tisa.
2
Kwani watu wa Beteli walimtuma Sareseri na Regemu-Meleki na watu wao kuja kumnyenyekea Bwana
3
na kuwauliza watambikaji waliomo Nyumbani mwa Bwana Mwenye vikosi na kuwauliza nao wafumbuaji kwamba: Tuomboleze katika mwezi wa tano na kujinyima menginemengine, kama tulivyofanya hii miaka yote iliyopita?
4
*Ndipo, neno la Bwana Mwenye vikosi liliponijia la kwamba:
5
Waambie watu wote wa nchi hii nao watambikaji kwamba: Kama mmefunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba hii miaka 70, je? Mmefunga kwa ajili yangu mimi?
6
Tena kama mnakula au kama mnakunywa, Je? Sio ninyi wenyewe mnaokula, tena mnaokunywa?
7
Yafaayo siyo yale maneno, Bwana aliyoyatangaza vinywani mwa wafumbuji wa kwanza, Yerusalemu ulipokuwa umekaa watu na kutulia vema, navyo vijiji vyake vilipouzunguka, nayo nchi ya kusini ilipokaa watu, hata nchi ya pwani?
8
Neno la Bwana likamjia Zakaria la kwamba:
9
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema kwamba: Kateni mashauri ya kweli yaliyo sawa, mhurumiane kila mtu na ndugu yake kwa kuoneana machungu!
10
Wajane nao waliofiwa na wazazi, nao wageni na wanyonge msiwakorofishe, wala mtu na ndugu yake msiwaziane mabaya mioyoni mwenu!*
11
Lakini walikataa kuyasikia hayo, wakawatolea kosi zao ngumu, wakayaziba masikio yao, wasisikie.
12
Wakaishupaza mioyo yao, iwe migumu kama almasi, wasiyasikie Maonyo wala maneno, Bwana Mwenye vikosi aliyoyatuma kwao kwa Roho yake na kuwatumia wafumbuaji wa kwanza. Ndipo, makali mengi yalipowajia toka kwa Bwana Mwenye vikosi.
13
Ikawa hivyo: kama wao walivyokataa kusikia, alipowaita, ndivyo, nami nilivyokataa kuwasikia, waliponiita; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
14
Kwa hiyo nimewatawanya kwa nguvu kama za upepo mkali katika wamizimu wote, wasiowajua, nchi nayo ikageuka nyuma yao kuwa mapori tu, asipatikane mtu aliyeipita wala kwa kwenda wala kwa kurudi. Hivyo ndivyo, walivyoigeuza nchi hii nzuri mno kuwa mapori matupu.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14