bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Zechariah 2
Zechariah 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 3 →
1
Nilipoyainua macho yangu, nichungulie, mara nikaona mtu, naye alishika mkononi mwake kamba ya kupimia.
2
Nikamwuliza: Unakwenda wapi? Akaniambia: Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione, upana wake na urefu wake ulivyo.
3
Mara malaika aliyesema na mimi akatoka, kisha malaika mwingine akatokea kukutana naye,
4
akamwambia: Piga mbio, umwambie yule kijana kwamba: Yerusalemu utakaa watu pasipo boma kwa wingi wa watu na nyama watakaokuwamo mwake.
5
Kisha mimi nitakuwa boma la moto litakalouzunguka nao utukufu wake uliomo mwake utakuwa mimi; ndivyo, asemavyo Bwana.
6
Ndivyo, asemavyo Bwana: Haya! Haya! Kimbieni, mwitoke nchi hiyo ya kaskazini! Kwani nimewatawanya ninyi katika pande zote nne za upepo wa angani; ndivyo, asemavyo Bwana.
7
Haya! Jiponye, Sioni ukaaye kwake binti Babeli!
8
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kuutokeza utukufu amenituma kwa wamizimu walioziteka mali zenu ninyi, kwani anayewagusa ninyi huigusa mboni ya jicho lake.
9
Ndipo, mtakaponiona, nikiwapungia kwa mkono wangu; ndipo, wao watakapokuwa mateka yao walio watumwa wao, mpate kujua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma.
10
Shangilia kwa furaha, binti Sioni! Kwani utaniona, nikija kukaa katikati yako; ndivyo, asemavyo Bwana.
11
Siku hiyo itakuwa, wamizimu wengi waje kuandamana na Bwana; ndipo, wao nao watakapokuwa ukoo wangu. Nitakaa katikati yako, upate kujua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma kwako.
12
Ndipo, Bwana atakapowatwaa Wayuda, wawe fungu lake katika nchi hii takatifu, nao Yerusalemu atauchagua tena, uwe mji wake.
13
Wote wenye miili ya kimtu sharti wanyamaze kimya usoni pake Bwana, kwani amekwisha kuondoka katika Kao lake takatifu!
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14