bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Zechariah 6
Zechariah 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 7 →
1
Nilipoyainua macho yangu tena, nichungulie, mara nikaona magari manne yaliyotoka katikati ya milima miwili, nayo milima hiyo ilikuwa ya shaba.
2
Gari la kwanza lilikuwa na farasi wekundu, gari la pili lilikuwa na farasi weusi,
3
gari la tatu lilikuwa na farasi weupe, gari la nne lilikuwa na farasi wenye nguvu, miili yao ilikuwa ya madoadoa.
4
Nikaanza kusema na kumwuliza malaika aliyesema na mimi: Hao maana yao nini, Bwana wangu?
5
Malaika akajibu, akaniambia: Hawa ndio pepo nne za mbinguni zinazotaka kutoka sasa kwa kuwa zimekwisha kusimama kwake Bwana wa nchi hii yote nzima.
6
Gari lenye farasi weusi linatoka kwenda katika nchi ya kaskazini, nao weupe wanalifuata. Wale wenye miili ya madoadoa wanatoka kwenda katika nchi ya kusini.
7
Nao wenye nguvu wanatoka kujitafutia mahali pa kwendea, wapate kutembea katika nchi. Alipowaambia: Haya! Nendeni katika nchi! ndipo, walipokwenda kutembea katika nchi.
8
Kisha akapaza sauti na kuniita, akaniambia kwamba: Tazama, hawa wanaotoka kwenda katika nchi ya kaskazini wataituliza roho yangu katika nchi ya kaskazini.
9
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
10
Watoze tunzo waliotekwa na kuhamishwa, akina Heldai na Tobia na Yedaya, ukija wewe mwenyewe siku hiyo kuingia nyumbani mwa Yosia, mwana wa Sefania, walimofikia walipotoka Babeli!
11
Tunzo utakalowatoza ni fedha na dhahabu; kisha fanya taji, kamvike mtambikaji mkuu Yosua, mwana wa Yosadaki, kichwani!
12
Umwambie kwamba: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema kwamba: Tazama, yuko mtu atakayekuja, jina lake Chipukizi, maana atachipukia mahali pake; ndiye atakayelijenga Jumba la Bwana.
13
Kweli yeye ndiye atakayelijenga Jumba la Bwana na kujipatia utukufu; atakaa katika kiti chake cha kifalme na kutawala, tena atakuwa mtambikaji katika kiti chake cha kifalme, nalo shauri, hao wawili watakalolipiga, litakuwa la mapatano.
14
Nazo hizo taji na zikae katika Jumba la Bwana kuwa ukumbusho wa Helemu na wa Tobia na wa Yedaya na wa Heni, mwana wa Sefania.
15
Nao walioko mbali watakuja kusaidia kulijenga Jumba la Bwana. Ndipo, mtakapojua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma kwenu. Haya yatatimia, mkiisikia sauti ya Bwana Mungu wenu na kuitii.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14