bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Zechariah 13
Zechariah 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 14 →
1
Siku hiyo ndipo, walio wa mlango wa Dawidi nao wenyeji wa Yerusalemu watakapofunuliwa kisima kwa ajili ya makosa na kwa ajili ya machafu.
2
Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku hiyo ndipo, nitakapoyang'oa majina ya vinyago vyote katika nchi hii, visikumbukwe tena; hata wafumbuaji na roho zenye uchafu nitawaondoa, watoke katika nchi hii.
3
Itakuwa, kama mtu atataka kufumbua maneno tena, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia: Hutapata kuishi, kwani unasema uwongo na kulitaja Jina la Bwana, kisha baba yake na mama yake waliomzaa watamchoma kwa ajili ya ufumbuaji wake.
4
Siku hiyo ndipo, wafumbuaji watakapopatwa na soni, kila mmoja kwa ajili ya maono yake, atakapofumbua maneno, tena hatakuwako atakayevaa joho la manyoya ya nyama, apate kusema yaliyo uwongo.
5
Ila atasema: Mimi si mfumbuaji, mimi ni mtu alimaye shamba, kwani tangu ujana wangu mtu alininunua, niwe mtumwa wake.
6
Mtu atakapomwuliza: Haya makovu kifuani katikati ya mikono yako ni ya nini? atasema: Ni ya mapigo, niliyoyapata nyumbani mwao, niliowapenda.
7
Wewe upanga, amka, umpige mchungaji wangu na mwenzangu wa bia! Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi. Mpige mchungaji, kondoo watawanyike! Nami nitaugeuza mkono wangu, uwaelekeze wadogo.
8
Ndivyo, asemavyo Bwana: Hapo ndipo, mafungu mawili yatakapoangamizwa katika nchi hii yote nzima, yafe, lakini fungu la tatu litasazwa huko.
9
Nalo hilo fungu la tatu nitalitia motoni, niwang'aze kwa kuwayeyusha, kama watu wanavyong'aza fedha kwa kuiyeyusha, tena nitawajaribu kabisa, kama watu wanavyojaribu dhahabu. Kisha hapo, watakapolililia Jina langu, mimi nitawaitikia na kuwaambia: Hawa ndio walio ukoo wangu; ndipo, watakapoitikia wao: Nawe Bwana ndiwe Mungu wetu.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14