bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Zechariah 3
Zechariah 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 4 →
1
Kisha akanionyesha mtambikaji mkuu Yosua, akisimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Satani alikuwa amesimama kuumeni kwake kumsengenya.
2
Bwana akamwambia Satani: Bwana na akukemee wewe, Satani! Yeye Bwana aliyeuchagua Yerusalemu, uwe mji wake, na akukemee wewe! Kumbe huyu si kijinga kilichopona kwa kuokolewa motoni!
3
Naye Yosua alikuwa amevaa nguo chafu aliposimama mbele ya malaika.
4
Kisha huyu akasema na kuwaambia waliosimama mbele yake kwamba: Mvueni hizi nguo chafu! Akamwambia: Tazama, manza, ulizozikora, nimeziondoa kwako, nikakuvika nguo za sikukuu.
5
Kisha akasema: Mfungeni kilemba kilichotakata kichwani pake! Wakamfunga kilemba kilichotakata kichwani pake pamoja na kumvika zile nguo, naye malaika wa Bwana alisimama papo hapo.
6
Kisha malaika wa Bwana akamshuhudia Yosua kwamba:
7
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kama utakwenda katika njia zangu na kuutumikia utumishi wangu, ndipo, wewe utakapoitunza Nyumba yangu na kuzilinda nyua zangu, kisha nitakupatia njia ya kufika kwangu katikati yao hawa wanaosimama hapa.
8
Sasa sikia, wewe mtambikaji mkuu Yosua pamoja na wenzako wanaokaa mbele yako, kwani ndio watu wa kutazamiwa: Mtaniona, nikimleta mtumishi wangu Chipukizi.
9
Kwani tazameni: Jiwe hili, nililoliweka mbele yake Yosua, macho saba yanalielekea jiwe hili moja; tena tazameni: Mimi ninachora humo machoro yanayolipasa, kisha nitaziondoa manza za nchi hii katika siku moja; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
10
Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Siku hiyo ndipo, watakapoalikana mtu na mwenziwe kuja kukaa pamoja chini ya mzabibu na chini ya mkuyu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14