bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
1 Chronicles 19
1 Chronicles 19
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 20 →
1
Nyuma ya hayo, Nahasi mufalme wa Waamoni akakufa, na mwana wake Hanuni akatawala kwa pahali pake.
2
Basi, Daudi akasema: “Nitamutendea mema Hanuni mwana wa Nahasi, maana baba yake alinitendea mema vilevile.” Halafu Daudi akatuma wajumbe na kumupelekea salamu za pole kwa ajili ya kifo cha baba yake. Nao wakaenda kwa Hanuni kwa kumufariji, kule katika inchi ya Waamoni.
3
Lakini viongozi wa Waamoni wakamwambia mufalme: “Unazani ni kwa sababu ya heshima ya baba yako ndiyo maana Daudi anatuma wajumbe hawa wakuje kukufariji? Watu hawa ni wapelelezi waliotumwa kuja kuichunguza inchi kwa kuiangamiza na kuipeleleza.”
4
Basi Hanuni aliwatwaa wajumbe wale wa Daudi, akawanyoa ndevu na kupasua nguo zao katikati mpaka kwenye matako, kisha akawaacha waende zao,
5
nao wakaondoka na kurudi kwao. Daudi alipopashwa habari jinsi wajumbe wake walivyotendewa, akatuma watu kwa kuwapokea maana wale wajumbe waliona haya sana. Naye mufalme akawaambia: “Mukae katika muji wa Yeriko, mpaka mutakapoota ndevu, kisha murudi.”
6
Waamoni walipoona wamejifanya wachukizwe na Daudi, Hanuni na wale Waamoni wakatuma watu wapeleke kilo elfu makumi tatu za feza kwa kulipa magari ya vita na waaskari wapanda-farasi kutoka Mesopotamia, Aramaka na Zoba.
7
Walikopesha magari elfu makumi tatu na mawili, na mufalme wa Maka na waaskari wake akakuja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni walikusanyika toka kwenye miji yao yote, wakajiweka tayari kwa vita.
8
Naye Daudi aliposikia habari hizo akatuma Yoabu na kundi lote la waaskari mashujaa.
9
Waamoni wakatoka na kujipanga kwenye mulango wa muji, wakati wale wafalme waliokuja walikuwa peke yao kwenye mbuga.
10
Yoabu alipoona kwamba vita ni kali juu yake, mbele na nyuma, akachagua waaskari hodari zaidi kati ya Waisraeli, akawapanga mbele ya Waaramu.
11
Wale waaskari wengine waliobaki, akawaweka chini ya uongozi wa ndugu yake Abisai, naye akawapanga waangaliane na Waamoni.
12
Yoabu akamwambia Abisai: “Ikiwa Waaramu wananizidi nguvu, utanisaidia; lakini kama Waamoni wanakuzidi nguvu, nitakuja kukusaidia.
13
Basi ukuwe hodari! Tupigane kama wanaume kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; na Yawe atutendee sawa na mapenzi yake.”
14
Basi, Yoabu na watu wake walisonga mbele kwa kupigana na Waaramu, nao Waaramu wakakimbia.
15
Waamoni walipoona Waaramu wamekimbia, nao walimukimbia Abisai, ndugu ya Yoabu, wakaingia katika muji. Halafu Yoabu akarudi Yerusalema.
16
Lakini Waaramu walipoona kwamba wameshindwa na Waisraeli, wakatuma wajumbe waende kuwaleta Waaramu wengine waliokuwa ngambo ya muto Furati wakiongozwa na Sofaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri.
17
Daudi alipopata habari, akakusanya pamoja Waisraeli wote, akavuka muto Yordani, akawaendea, akapanga vikundi vyake mbele yao. Daudi alipopanga vita juu ya Wasuria, basi nao wakapigana naye.
18
Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Waisraeli. Daudi akawaua Waaramu wanaoendesha magari elfu saba na waaskari wa miguu elfu makumi ine. Vilevile akamwua Sofaki, jemadari wa jeshi lao.
19
Kisha watumishi wa Hadadezeri walipoona kwamba wameshindwa na Waisraeli, wakafanya mapatano ya amani na Daudi nao wakakuwa watumishi wa Daudi. Halafu Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29